NDJAMENA: Hali ya hatari imetangazwa kufuatia machafuko ya kikabila | Habari za Ulimwengu | DW | 14.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NDJAMENA: Hali ya hatari imetangazwa kufuatia machafuko ya kikabila

Chad imetangaza hali ya hatari katika mji mkuu N´djamena na maeneo ya mashariki.Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia machafuko ya kikabila yaliosababisha vifo vya watu mia kadhaa katika majuma machache yaliopita.Serikali imewatuhumu wanamgambo wa Kisudan walio na asili ya Kiarabu kuwa ndio waliochochea mapambano kati ya Wachad wenye asili ya Kiarabu na wale wasio na asili ya Kiarabu.Wanamgambo hao wametuhumiwa kuwa mara kwa mara wamevamia eneo la mashariki la Chad linalopakana na jimbo la mgogoro la Darfur nchini Sudan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com