1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yajadili mfuko wa yuro bilioni 100 kwa Ukraine

3 Aprili 2024

NATO imejadili leo mpango wa kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine kwa siku zijazo ikiwa Urusi itaendelea kuchukua udhibiti huku ikijadili pia mpango wa mfuko wa yuro bilioni 100 wa miaka mitano kuisadia Ukraine

https://p.dw.com/p/4eOuG
Jens Stoltenberg , Blinken
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akiwa anateta jambo na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anton BlinkenPicha: Johanna Geron/Reuters/AP/picture alliance

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama ya NATO wako mjini Brussels leo kujadili mpango wa kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine kwa siku zijazo ikiwa Urusi itaendelea kuchukua udhibiti katika vita vinavyoendelea, mbali na hilo mawaziri hao pia wamejadili pendekezo la kuunda mfuko wa euro bilioni 100 wa miaka mitano kwa ajili ya kuisadia Ukraine.

Soma zaidi. Mawaziri wa mambo ya nje wa NATO wajadili msaada kwa Ukraine

Mataifa wanachama ya NATO yanajadili juu ya namna ya kuondokana na utaratibu wa kutoa misaada ya muda mfupi kwa Ukraine na badala yake kutengeneza mpango wa ahadi za muda mrefu zitakalolisaidia taifa hilo lililopo kwenye vita.

 | Jens Stoltenberg
Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa NATOPicha: Dursun Aydemir/Anadolu/picture alliance

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg akiwaongoza mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa hya jumuiya hiyo mjini Brussels kwamba Ukraine imepunguza umri wa kuingia jeshini kutoka miaka 27 hadi 25 ili kuongeza safu yake ya kijeshi inayozidi kupungua kutokana na vita vya Urusi nchini humo.

Ukraine kupokea msaada wa NATO

Jumuiya hiyo inapanga kutoa msaada zaidi wa silaha za kijeshi, na mahitaji mengine muhimu kwa Ukraine ili kuisaidia kuongeza nguvu katika uwanja wa mapambano, Jumuiya hiyo inatajwa kuwa tayari kuisadia kikamilifu Ukraine ingawa  baadhi ya wanachama wake hawako tayari kutoa dhamana hiyo.

Baadhi ya nchi wanachama za NATO zinaamini kuwa kufanya hivyo kutapelekea vita kubwa zaidi na hofu kwamba Urusi inaweza kuingia kwenye hatari kutumia silaha za nyukilia.

Soma zaidi. Putin: Sina mipango ya kushambulia mataifa ya NATO

Maafisa hao wamependekeza kuundwa kwa mfuko wa euro bilioni 100 wa miaka mitano kusaidia Ukraine, mpango ambao umeungwa mkono kikamilifu na mataifa ya Poland na mataifa ya baltiki.

Ukraine- Donetsk
Picha ya eneo la Donetsk huko Ukraine lililoharibiwa na shambulizi la UrusiPicha: ALEXANDER ERMOCHENKO/REUTERS

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa mambo ya nje wa Canada, Melanie Joly amesema msaada kwa Ukraine ni jambo la kupewa kipaumbele.

''Kwa hivyo tulitaka kuhakikisha kwamba Ukraine inaweza kupata uhakikisho huu wa usalama, dhamana hizi, hadi kuwa mwanachama wa NATO. Na ndio maana tunaendelea kukaribisha aina yoyote ya msaada ambayo Ukraine inaweza kuwa nayo, kwa sababu tunahitaji kutuma ujumbe kwa watu wa Ukraine wenyewe. Lakini pia tunahitaji kutuma ujumbe kwa Urusi."

Soma zaidi. Tume ya uchaguzi yapigilia msumari ushindi wa Putin

Kando ya mkutano huo, mawaziri wa mambo ya nje wa NATO pia walitarajiwa kujadili kinyang'anyiro cha kuchukua nafasi ya Jens Stoltenberg, ambaye muda wake wa muongo mmoja unamalizika mwezi Oktoba.

Rais wa Romania Klaus Lohannis na Waziri Mkuu wa Uholanzi  Mark Rutte wanatarajiwa kuwa washindani wakuu wa kinyanganyiro hicho.