NAJAF: Watu takriban 300 wauawawa karibu na mji wa Najaf | Habari za Ulimwengu | DW | 29.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAJAF: Watu takriban 300 wauawawa karibu na mji wa Najaf

Polisi nchini Irak wanasema vikosi vya usalama vya Irak na Marekani vimewaua wapiganaji 300 karibu na mji mtakatifu wa Najaf. Mapigano yameendelea leo kati ya wanajeshi wa Irak wakisaidiwa na wanajeshi wa Marekani dhidi ya wanamgambo wa kundi lisilojulikana tangu mapigano yalipozuka hapo jana kaskazini mwa Najaf.

Imeripotiwa kwamba wanajeshi watatu wa Irak wameuwawa katika mapigano hayo. Jeshi la Marekani limesema wanajeshi wawili waliuwawa wakati helikopta yao ilipotunguliwa.

Gavana wa eneo hilo amesema wanamgambo hao walipania kuwashambulia mashehe wa kishia hii leo huku mahujaji wakiendelea kukusanyika kwa maombolezi ya Ashura.

Usalama umeimarishwa katika mji Najaf kuzuia kuzuka kwa machafuko.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com