NAIROBI : Ukuta waangukia nyumba na kuuwa 10 | Habari za Ulimwengu | DW | 10.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI : Ukuta waangukia nyumba na kuuwa 10

Ukuta wa kangriti umeangukia mparaganyiko wa nyumba hapo Jumamosi usiku katika kitongoji duni nchini Kenya na kuuwa takriban watu 10 wakiwemo watoto wachanga watatu.

Julius Muthuri mkuu wa polisi katika eneo la mji mkuu wa Nairobi unaojumuisha kitongoiji duni cha Mukuru amesema inaonekana ukuta huo umeanguka baada ya mvua kubwa kudhoofisha msingi wake.Amesema walikuwa wakiondowa vifusi kuona iwapo kuna maiti zaidi.

Ukuta huo ulikuwa ukitumika kama uzio katika mtaa huo wa mabanda ambapo nyumba zake zimejengwa kwa mbao na mabati yaliokunjana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com