1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa madeni wahatarisha umoja barani Ulaya

13 Oktoba 2011

Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya umeahirishwa hadi Oktoba 23 kwani Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa wanataka muda zaidi kutafuta suluhisho la mzozo wa madeni barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/RqeC
Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) und der franzoesische Staatspraesident Nicolas Sarkozy kommen am Sonntag (09.10.11) zu einer Presseunterrichtung nach ihrem Gespraech im Bundeskanzleramt in Berlin. (zu dapd-Text) Foto: Steffi Loos/dapd
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani (shoto) na Rais Nicolas Sarkozy wa UfaransaPicha: dapd

Viongozi hao wawili wanashirikiana na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy kupata suluhisho hilo. Hata hivyo, itakuwa shida kuutekeleza mpango wo wote utakaoandaliwa, kwani mzozo wa madeni umeathiri mshikamano wa kanda ya euro na Umoja wa Ulaya. Tangu mzozo wa fedha na madeni kuzuka barani Ulaya, nchi 7 kutoka wanachama 17 wa kanda ya euro, zimepata serikali mpya. Katika nchi tatu zingine, chaguzi mpya zinatazamiwa kufanywa, Slovakia ikiwa mojawapo. Serikali ya mseto nchini Slovakia, ilivunjika mapema wiki hii kwa sababu ya mvutano uliozuka kuhusiana na mpango wa kuongeza fedha katika mfuko wa kuzisaidia nchi zenye madeni katika kanda ya euro.

Italian Premier Silvio Berlusconi, right, speaks to his supporters outside Milan's courthouse where he attended his trial on tax fraud charges, Italy, Monday, April 11, 2011. Berlusconi said attending a hearing of his tax fraud trial in Milan was a waste of time and resources, accusing prosecutors of having no case against him. (AP Photo/Luca
Waziri Mkuu wa Italia, Silvio BerlusconiPicha: AP

Nako Italia, Rais Giorgio Napolitano ametambua kuwa serikali ya Waziri Mkuu Silvio Berlusconi haina uwezo wa kutawala. Nchini Ufaransa, Rais Nicolas Sarkozy amepoteza wingi wake katika baraza la Seneti na anapaswa kuitisha uchaguzi mwakani. Mzozo huo wa madeni barani Ulaya, umesababisha mvutano katika serikali ya mseto ya Ujerumani ya vyama vya CDU,CSU na FDP. Ubeligiji kuna serikali inayoshughulikia masuala ya uongozi tu na Uholanzi serikali inatawala kwa wingi mdogo tu. Katika kanda ya Euro, kimamlaka ni nchi nne tu zilizo imara. Hizo ni Luxembourg, Austria, Estonia na Malta. Sura hiyo inadhihirisha jinsi ilivyokuwa vigumu kuchukua hatua za kuumaliza mzozo wa madeni, wakati ambapo kila mara, viongozi wepya wa serikali hushiriki katika mikutano hiyo.

Mtaalamu wa masuala ya fedha wa chama cha Social Demokrat katika bunge la Ulaya Udo Bullmann anasema tatizo ni kwamba kunakosekana viongozi wa kueleza hatua zinazopaswa kuchukuliwa. Anasema:

"Serikalini kuna viongozi wachache walio na ujasiri wa kutamka waziwazi hatua ngumu zinazopaswa kuchukuliwa, ili kuhakikisha mustakabali ulio bora."

### Achtung Redaktionen, es gibt keine aktuellen Bilder von Barroso zur Stellungnahme der EU zum Tod Bin Ladens, dieses ist das aktuellste von ihm! ### European Commission President Jose Manuel Barroso during a news conference in Kiev, Ukraine, Monday, April 18, 2011. (AP Photo/Sergei Chuzavkov)
Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel BarrosoPicha: AP

Hata Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso, ana wasiwasi kuwa ushawishi wa chombo hicho muhimu cha uongozi, umepungua, kwani maamuzi ya dharura na kuhusu mfuko wa kuzisaidia nchi zenye madeni, yameptishwa na serikali za nchi wanachama bila ya kuzishirikisha taasisi za umoja huo. Kwa hivyo, Barosso ameshauri kuwa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya kiwe chombo cha kusismamia masuala ya kiuchumi na pia taasisi zilizokuwepo ziimarishwe.

" Njia pekee ni kuwa na mageuzi, ushirikiano zaidi na uongozi bora wa Ulaya ili kuweza kuamini uwezo wetu wa kuwajibika."

Jose Barosso anataka usimamizi bora zaidi wa sera za uchumi na malipo ya kodi katika nchi wanachama 17 katika kanda ya euro.

Hata hivyo wataalamu wa masuala ya fedha wanaamini umoja wa sarafu na kanda ya euro zitaweza kufanya kazi ikiwa itakubaliwa kupunguza madeni ya Ugiriki, kurejesha utulivu katika benki za Ulaya na kuwa na mfuko wenye fedha za kutosha kuzinusuru Italia na Uhispania.

Mwandishi: Riegert,Bernd/zpr

Mhariri: Mohammed Khelef