1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanajeshi wa Bahrain wauwa katika shambulio la droni

Saumu Mwasimba
26 Septemba 2023

Kamandi ya kijeshi ya Bahrain imefahamisha kwamba shambulio lililofanywa na waasi wa Kihouthi wa Yemen kwa kutumia ndege isiyoendeshwa na rubani limemuuwa afisa mmoja na mwanajeshi wa Bahrain jana.

https://p.dw.com/p/4Woim
Baadhi ya wanajeshi wa jeshi la Bahrain wakiwa katika majukumu yao
Baadhi ya wanajeshi wa jeshi la BahrainPicha: dapd

Taarifa ya jeshi iliyorushwa na shirika la habari la serikali ya Bahrain imesema wanajeshi wengine kadhaawa nchi hiyo walijeruhiwa katika shambulio hilo, ingawa haikutowa ufafanuzi. 

Soma pia:Bahrain yasema wanajeshi wake wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulizi la ndege isiyotumia rubani

Shambulizi hilo lilifanywa na waasi wa Kihouthi wakilenga maeneo waliyoko walinzi wa Bahrain katika eneo la mpaka wa kusini kati ya Saudi Arabia na nchi hiyo. 

Shambulio hilo pia limefanyika kukiwa na makubaliano ya kusitisha kwa operesheni za kijeshi kati ya pande zinazohasimiana nchini Yemen.