1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBahrain

Bahrain na Israel kuimarisha ushirikiano wao

4 Septemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Israel amefikia makubaliano na mwenzake wa Bahrain ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara baina ya nchi zao.

https://p.dw.com/p/4Vwm5
Bahrain | Abdullatif bin Rashid Alzayani und Eli Cohen
Waziri wa Mambo ya Nje Bahrain r Abdullatif bin Rashid Alzayani na mwenzake wa Israel Eli Cohen.Picha: Bahrain Ministry of Foreign Affairs/AA/picture alliance

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa ziara ya kwanza ya waziri huyo wa Israel katika nchi hiyo ambayo ni miongoni mwa nchi mbili za Ghuba ya Kiarabu zilizoanzisha mahusiano na Israel.

Katika sherehe ya ufunguzi wa ubalozi mpya wa Israel mjini Manama,waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Eli Cohen alisema yeye pamoja na mwenzake wa Bahrain wamekubaliana kushirikiana kuongeza idadi ya safari za ndege za moja kwa moja baina ya nchi zao,kiwango cha utalii pamoja na biashara na uwekezaji. 

Soma pia:Waziri wa mambo ya nje wa Israel azuru Bahrain

Cohen aliwasili JumapiliBahrain akiandamana na ujumbe wa wafanyabiashara wa makampuni zaidi ya 30 kutoka sekta ya Teknolojia za kisasa,usafiri na ujenzi wa majumba.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW