Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo limepitisha mswaada wa kutoa msamaha kwa waasi wa mikoa ya Kivu ya kusini na Kaskazini.
Hata hivyo, hatua hiyo haijawaridhisha wanamgambo wa mkoa wa Ituri.Kutokana na hali hiyo kiongozi wa UPC, ameelezea kuwa ilibidi wanamgambo wa Ituri wapatiwe nao msamaha ili waliosalia msituni nao watoke huko.
Kutoka Beni Mwandishi wetu John Kanyunyu anaripoti zaidi