1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshukiwa wa kundi la Alshabaab ashtakiwa Ujerumani

Caro Robi
14 Mei 2018

Waendesha mashtaka wa Ujerumani wamemfungulia mashitaka mwanamume mmoja kutoka Somalia anayedaiwa kuwa mwanachama wa kundi la wanamgambo wa Al Shabab

https://p.dw.com/p/2xfp3
Somalia Al-Shabaab Kämpfer
Picha: picture alliance/AP Photo/F. A. Warsameh

Maafisa nchini Ujerumani wamemfungulia mashitaka mwanamume mmoja kutoka Somalia anayedaiwa kuwa mwanachama wa kundi la waasi la Al Shabab anayetuhumiwa kufanya jaribio la mauaji na kusaidia katika mauaji. Waendesha mashitaka wa Ujerumani wamesema mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 20 anayetambulika kwa jina Abduqaadir A alijiunga na kundi hilo la waasi mwaka 2012 mjini Mogadishu na alipewa mafunzo ya kutumia bastola na magureneti.

Wakati wa mafunzo hayo, inadaiwa mshukiwa huyo aliandamana na wanachama wengine wa Al Shabab kwenda msikiti ambako walimuua mtu mmoja kwa kumpiga risasi tatu kichwani. Baadaye aliagizwa kumuua afisa mmoja wa serikali ya Somalia katika mkahawa mmoja. Alifanikiwa kutoroka Somalia mwezi Okotoba mwaka 2012 na alikimbilia Ujerumani mwaka 2014 kabla ya kukamatwa mwezi Februari mwaka huu.