1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Urusi haiungi mkono matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya Iran

18 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOf

Waziri wa mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema kuwa nchi hiyo imeguswa na mapendekezo yaliyotolewa ya matumizi ya kijeshi dhidi ya Iran.

Alikuwa akijibu matamshi ya Waziri mwenzake wa nje wa Ufaransa Bernard Kouchner aliyotoa Jumapili iliyopita ya kwamba kuna hatari ya vita dhidi ya Iran kuhusiana na mpango wake wa nuklia.

Lavrov alisema hayo baada ya mazungumzo yake na Kouchner mjini Moscow ambapo alisema matumzi ya nguvu za kijeshi katika eneo ambalo tayari lina matatizo ni matokeo ya kubahatisha.

Maafisa wa Marekani mara kadhaa wamekuwa wakirejelea kauli zao ya kwamba njia zote za kuutanzua mzozo huo wa mtambo wa nuklia wa Iran zikiwemo za mashambulizi ya kijeshi ziko tayari kutumika.