Moscow.Sergei Lavrov audharau mswaada mpya wa Azimio la Umoja wa Mataifa. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Moscow.Sergei Lavrov audharau mswaada mpya wa Azimio la Umoja wa Mataifa.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amenukuliwa akisema kuwa, mswaada mpya wa azimio la Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran hauna maana yoyote katika kulishughulikia suala la mvutano wa kinyuklia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi Interfax, Lavrov amesema, mapendekezo ya mwisho yameshindwa kuorodhesha malengo yatakayohakikisha kuwa Tehran haitajipatia teknolojia tete ya kinyuklia na wakati huo huo kuwacha wazi njia zote za majadiliano.

Mswaada wa mwisho uliowasilishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi za Umoja wa Ulaya utajadiliwa baadae hii leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com