MOSCOW:Mzozo wa Georgia na Urussi ndo kwanza wapanuka | Habari za Ulimwengu | DW | 04.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW:Mzozo wa Georgia na Urussi ndo kwanza wapanuka

Katika mzozo wa hivi karibuni kati ya Urussi na Georgia,rais Vladmir Putin ameishutumu Georgia kwa kuchukua hatua za uchokozi na za kisaliti dhidi ya nchi yake.

Rais Putin akitoa matamshi makali juu ya Georgia amesema.

‘’Nisingemshauri mtu yoyote kutumia lugha ya uchkozi na kukandamiza dhidi ya Urussi.

Kufuatia hali hii bunge la mjini Moscow linaandaa mswaada unaoushutumu utawala wa Georgia unaounga mkono nchi za magharibi.Maafisa wa Georgia awali waliitaka Urussi iwaondoe wanajeshi wake karibu na mpaka wa baharini baina ya nchi hizo mbili.

Mjumbe wa Georgia katika Umoja wa mataifa amesema kuwepo kwa wanajeshi hao wa Urussi katika eneo hilo ni kitisho kwa amani ya eneo zima na pia ni kinyume na makubaliano ya Umoja wa Mataifa.

Urussi hadi sasa imekataa kuzingatia matakwa ya Marekani na Umoja wa ulaya kwamba nchi hiyo ifute vikwazo vya kiuchumi na usafiri dhidi ya Georgia licha ya Gergia kuwaachilia huru maafisa wa Uruusi siku ya jumatatu.

Maafisa hao walikamatwa wiki iliyopita juu ya madai ya kuhusika na shughuli za kijasusi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com