1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Ndege za Urusi zapiga doria upya

Kwa mara ya kwanza tangu miaka 15,vikosi vya anga vya Urusi vimeanza kupiga doria katika ndege za kurusha makombora ya masafa marefu.Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema,ndege 14 zimeruka kutoka viwanja mbali mbali nchini humo.Amesema,hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu ya kitisho cha nchi za nje kinachozidi.

Akaongezea kuwa baada ya kusambaratika kwa Soviet Union ya zamani,usalama wa Urusi umeathirika.Putin akaeleza kuwa Moscow ilisitisha misafara ya ndege hizo,lakini mataifa mengine hayakufuata mfano huo.Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema,haina wasiwasi na uamuzi huo wa Moscow.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com