1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu:Watu wengi wanasemekana wameuwawa katika shambulio la ndege ya kijeshi ya Marekani kusini mwa Somalia.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHV

Maafisa wa serekali ya Somalia wamesema idadi kubwa ya watu wameuwawa katika shambulio la ndege liliofanywa na Marekani dhidi ya vituo vinavoshukiwa kuwa ni vya mtandao wa al-Qaida kusini mwa Somalia. Nani waliouliwa katika shambulio hilo hawajaweza kuhakikishwa, lakini maafisa wanasema malengo ya mashambulio hayo yalikuwa ni pamoja na kiongozi wa cheo cha juu wa mtandao wa al-Qaida katika Afrika Mashariki pamoja na mwanaharakati wa al-Qaida anayetafutwa kutokana na mashambulio ya mabomu yaliofanyiwa balozi za Marekani nchinI Kenya na Tanzania. Washukiwa hao waliofanya hujuma za mabomu wanaaminiwa wanahifadhiwa na Waislamu wenye itikadi kali nchini Somalia. Rais wa mpito wa Somalia, Abdullahi Yusuf Ahmed, ameyatetea mashambulio hayo yaliofanywa na Marekani. Huu ni ujiingizaji wazi wa kijeshi wa Marekani katika Somalia tangu mwanzoni mwa miaka ya tisini.