MOGADISHU:Mapigano Puntland na Somaliland | Habari za Ulimwengu | DW | 15.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU:Mapigano Puntland na Somaliland

Mapigano makali yameripotiwa kutokea kati ya majeshi ya eneo la Somaliland na eneo lililo na uwezo wa kujiongoza la Puntland.Kulingana na maafisa wa serikali ghasia hizo zilitokea jana jioni katika eneo la Dahar baada ya mzozo wa mpaka kuzuka.Pande zote mbili zinaripotiwa kutangaza kuwa wameshinda katika mapigano hayo ila idadi ya waliofariki bado haijulikani.

Majeshi hayo yalipambana kwa mara ya kwanza wikendi iliyopita kwasababu ya mzozo huohuo.Eneo la Somaliland lililomilikiwa na wakoloni wa Uingereza lilijitenga na Somalia mwaka 91 ikiwa ni miezi minne baada ya Mohamed Siad Barre kungolewa madarakani.

Eneo la Puntland lilitangaza kujiongoza mwezi Agosti mwaka 98 chini ya uongozi wa Abdullahi Yusuf Ahmed aliye Rais wa serikali ya muda ya Somalia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com