1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Waislamu wataka kupigana jihadi na Ethiopia.

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgl

Muungano wa mahakama za Kiislamu nchini Somalia umetoa wito kwa Waislamu kutoka mataifa ya nje kwenda kupigana vita vya kidini dhidi ya Ethiopia nchini humo. Sheikh Mahmud Ibrahim Suleym wa mahakama hizo amesema kuwa mzozo huo utaendelea hadi pale ambapo hakutakuwa na Waethiopia tena katika ardhi ya Somalia.

Ethiopia imekuwa ikikana kuwa imetuma majeshi nchini Somalia lakini imesema kuwa imetuma washauri wa kijeshi kuisaidia serikali dhaifu ya mpito kujilinda katika mji wa Baidoa.

Umoja wa mataifa umezitaka pande zote mbili kurejea katika meza ya majadiliano ya amani mjini Khartoum.