Mkutano wa Umoja wa Ulaya, Brussels.
29 Oktoba 2010Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuyaangalia kwa makini mapendekezo yaliyotolewa na Ujerumani, juu ya mfumo wa udhamini uliobuniwa kuzuia kutokea tena kwa msukosuko wa fedha, kama ule, uliotokea nchini Ugiriki mapema mwaka huu.
Hayo yamesema leo asubihi na kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Brussels, Ubelgiji kunakofanyika mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya.
Wanachama wa Umoja wa Ulaya wataamua juu ya jambo hilo, ifikapo mwezi Desemba.
Lakini mpango wenye utata, uliotolewa na Ujerumani na Ufaransa juu ya kuzuia haki ya kupiga kura, mataifa wanachama ambayo yatavunja sheria za bajeti za umoja huo, umeendelea kukosolewa vikali.
Mapendekezo yote yatakayojadiliwa katika mkutano huo wa siku mbili mjini Brussels, yatahitaji kufanyiwa mabadiliko kwa mkataba wa Lisbon wa umoja huo.