Mkutano wa masuala ya ustawi wa jamii ya Umoja wa Afrika nchini Ethiopia | Masuala ya Jamii | DW | 17.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Mkutano wa masuala ya ustawi wa jamii ya Umoja wa Afrika nchini Ethiopia

Kamisheni ya kazi na masuala ya ustawi wa jamii ya Umoja wa Afrika inafanya mkutano wake wa 5 wa kawaida mjini Addis Abeba nchini Ethiopia.

Kikao hicho kinahusisha wawakilishi wa serikali, vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kujadilia masuala mbalimbali ya kuimarisha ajira vile vile kupambana na changamoto zinazotokana na utandawazi.

Mwandishi wetu wa Addis Abeba Anaclet Rwegayura alizungumza na Dr.Aggrey Mulimba mkurugenzi mtendaji wa chama cha waajiri nchini Tanzania anayehudhuria mkutano huo wa siku tatu.