1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya

18 Juni 2009

Rais wa Time ya UU Barroso abidi kusubiri kwa awamu nyengine.

https://p.dw.com/p/ISkt
Angela Merkel na Barroso.Picha: picture-alliance/ dpa

Katika mkutano wa kilele wa Umoja was Ulaya baadae hii leo mjini Brussels, viongozi wa Umoja huo hawana azma ya kumpendekeza rasmi rais mpya wa Tume ya Umoja wa Ulaya.Kwavile, bado si wazi ni mkataba gani mwishoni mwa mwaka huu utatumika,kuteuliwa kwa rais mpya wa Tume ya Umoja wa Ulaya,kumetatanika.Rais wa sasa wa Tume hiyo, Bw.Barroso kutoka Ureno,inampasa sasa kungoja kuidhinshwa kwa kipindi cha pili.

Tume ya UU inayoendesha shughuli za utawala inahitaji rais wake mpya hapo Novemba.mwaka huu.Kwani, kipindi cha rais wa sasa wa Tume hiyo kinamalizika.Waziri-mkuu wa zamani wa Ureno, Jose Barroso pamoja na watumishi wake 20.000 wangependa kuendelea kwa kipindi kingine cha miaka 5.

Lakini, viongozi wa dola na serikali wa UU na hata Bunge la Umoja huo lililochaguliwa hivi karibuni wanapasa kumuidhinisha.Bw.barroso anatokana na tawi la vyama vya kikonservative-wahafidhina.Wingi mkubwa wa viongozi hao wa dola na serikali mjini Brussels, wanatokana na tawi la vyama hivyo na hata wabunge wa Ulaya wengi wao ni wahafidhina.

Kwahivyo, kuchaguliwa tena kwa Bw.Barroso kusingeonekana ku na matat yoyote,lakini wapi,kuna turufu zisizojulikana zitapigwa upande gani.Na hivyo, Bungeni Bw.Barroso sio tu anahitaji kura za wahafidhjina,waliberali bali pia hata za baadhi ya wasoshalisti.Kiongozi wa hadi sasa wa tawi la vyama vya wasoshalisti,Bw.Martin Schulz, anafahamika kuwa mpinzani mkali wa Bw.Barroso na ameshapendekeza asipigiwe kura.

Na hata tawi la wafuasi wa mazingiora-KIJANI-wanaandaa mkakati wa kumuangusha Bw.Barroso.Wangependa kumpendekeza mtetezi wao wenyewe,lakini hii haikubaliki kwani ni jukumu la viongozi wa dola na serikali kumpendekeza nani awe Rais wa Tume ya Ulaya.Katika hali ya kutatanisha kama hii, wanasiasa wa UU hufanya nini ?

Barabra, hujakosea: huamua kuahirisha uamuzi juu ya mtetezi kwa muda wa mwezi.Bw. Barroso binafsi, angependa sana hii hii leo kuidhinishwa madarakani,lakini hivyo haiwezekani .Viongozi wa dola na serikali wanataka sasa kushauriana Bungeni ili kuepusha kuangushwa kwa mtetezi wao Bw.Barroso.

Kuna pia uwezekano kwa Bunge la Ulaya likaahirisha uamuzi wake hadi mwishoni mwa mwaka huu.Madhumuni hapo, ni kungoja kuona iwapo na lini, ule mkataba wa mageuzi wa UU -mkataba wa Lisbon,utaanza kufanya kazi au la.

Mkataba wa Lisbon unaitisha kanuni mpya za kuunda tangu Tume ya UU hata rais wake.Kwa ilivyo wakati huu, Taasisi hizo ziundwe kwa muujibu wa kanuni za Mkataba wa Niece. Mkataba huo unasema Tume ya UU alao iwe na mtu mmoja kasoro kuliko idadi ya wsanachama wa Umoja wa Ulaya-hivyo ni kusema 26.Mwanachama mmoja wa Ulaya asipeleke mjumbe wake katika Tume hiyo mjini Brussels.

Kwa muujibu wa mkataba wa Lisbon,kila mwanachama anastahiki kuwa na mjumbe wake katika Tume hiyo tena kwa kipindi cha miaka 5 .Baadae Tume hiyo, ipungzwe kwa thuluthi-moja.Nchi ndogo-ndogo za Umoja huu, zinahimniza kuteuliwa kwa Tume mpya kuahirishwe kwa muda mrefu iwezekanavyo, ili asitokee mmoja wao kutobidi kutowakilishwa.Kwani, hakuna ajuwae,ni nchi gani baadae zitajiunga na Tume hiyo na zipi hazibidi kutuma wajumbe wao Brussels.Je, hii itaamuliwa kwa kura au kwa bahati nasibu ?Mkataba wa Niece haukusema iwe vipi.

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman