Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya Brussels | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.03.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya Brussels

Kuzidi kwa hali ya joto ulimwenguni ni mada kuu katika kikao cha leo na kesho katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya.na hii ni kinyume na ajenda ya kawaida ya viongozi wa nchi hizi 27.

Kanzela Angela Merkel ajikinga na mvua na sio moshi hapa.

Kanzela Angela Merkel ajikinga na mvua na sio moshi hapa.

Mkutano wa kilele wa viongozi wa dola na serikali wa Umoja wa ulaya wanakutana hii leo na kesho mjini Brussels,Ubelgiji.

Kwa desturi kikao hiki hujishughulisha na maswali ya kiuchumi na ya kijamii.Mara hii lakini,rais wa Umoja huu Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani,ameliweka usoni kabisa swali la ulinzi wa mazingira.

Kuzidi kwa ujoto ulimwenguni kunawaumiza vichwa sasa viongozi hawa .Na viongozi wote 27 wanakubaliana sasa kwamba hatua inabidi kuchukuliwa na hakuna wakati tena wa kupoteza.

Mabishano yako tu juu ya hatua gani zichukuliwe na hii ndio itakayokua mada motomoto leo hii mjini Brussels.Mwishoni mwa majadiliano lazima matokeo wazi yaibuke, kwani katika swali hili la mazingira uaminifu wa UU umo mashakani iwapo kweli umejiwinda barabara kusafisha mazingira.

Hali hii anataka kuibanisha wazi hata rais wa komisheni ya UU,Jose Manuel Barroso alipoweka wazi kabla kuanza mkutano wa kilele wa hili leo.

“Kuanzia Washington hadi Beijing, tutakodolewa macho na kuhukumiwa iwapo tunadhamiria kweli tunapozungumzia nishati ya usalama na ulinzi wa mazingira.

Maazimio ambayo viongozi wa dola na serikali wa UU watayopitisha hapa ,yataacha athari zake kupindukia mipaka ya Ulaya na hata kizazi kijacho.”

Shabaha kuu inayolengwa kuzuwia kupanda kwa hali ya ujoto duniani kwa kima cha wastani cha nyuzi 2.Kwa muujibu wa makisio ya Tume ya UU,inalengwa hadi ifikapo mwaka 2050 kupunguza moshi unaochafua hewa kwqa 50% na kuurejesha katika kipimo kilichokuwapo 1990.

UU una azma ya kupiga mfano mwema kama alivyoweka wazi mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya wiki iliopita Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani.

“Ninaungamkono kanuni isemayo moshi unaochafua hewa kutoka nchi za Umoja wa ulaya, upunguzwe kwa kima cha 20% hadi ifikapo mwaka 2020.Lakini sitaki kuficha kuwa shabaha hiyo ni ngumu kuifikia.”

Moshi wenyewe unaolengwa hapo kupunguzwa ni ule co2 unaotoka kwenye magari.Hadi mwaka 2012 moshi huu ndani ya nchi za UU kutoka kiwango cha hivi sasa cha g 186 cha wastani kukiteremsha hadi g 120 kwa kila km 1.

Mashirika yanayotetea mazingira safi yanapigania viwanda vinavyounda magari viwajibike kwa kuweka vipimo maalumu vya chini.Hapa lakini, viwanda vikubwa vya magari vya Ujerumani na vyenye sauti vinazusha ubishi.

Ala nyengine ya kupambana na uchafuzi wa hali ya hewa kwa kupunguza moshi , ni kutumiwa zaidi nishati inayoweza kutumika tena na tena”renewable energy”.

Kipimo cha nishati hii katika matumizi jumla ndani ya UU ni 6.5%.Ujerumani kwa kima chake cha 5,3 % iko hata chini ya kima cha wastani kinachotakiwa.Katika mkutano wa leo na kesho wa viongozi wa UU, Bibi Angela Merkel, amepania kwhivyo kuona kiwango cha nishati hii inayoweza kutumika tena na tena kinapanda hadi 20% ifikapo 2020.

 • Tarehe 08.03.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHIg
 • Tarehe 08.03.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHIg

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com