1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa hali ya hewa mjini Paris

Oummilkheir1 Februari 2007

Ripoti ya IPCC yaonya dhidi ya madhara ya kuzidi hali ya ujoto ulimnwenguni

https://p.dw.com/p/CHKw
Theluji yayayuka huko Groenland
Theluji yayayuka huko GroenlandPicha: AP

Mabadiliko ya hali ya hewa yatapelekea kuenea ukame , kuzidi mafuriko,vimbunga , kupanda kina cha maji ya bahari na kusababisha wimbi la mamilioni ya wakimbizi katika kipindi cha miongo kadhaa ijayo-hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya wataalam waliokua wakikutana mjini Paris kutahmini madhara ya kuzidi ujoto ulimwenguni.

Wataalam Zidi ya 450 wa tume ya mashirika yanayoshuguhulikia mabadiliko ya hali ya hewa-IPCC wametangaza ripoti yao ya nne ya ya kisayansi hii leo mjini Paris.Ripoti hiyo ni matokeo ya uchunguzi na utafiti uliofanywa na zaidi ya wataalam 2500 kutoka zaidi ya nchi 130 za dunia.

Ripoti hiyo inatoa picha ya kutisha ya maafa yanayoweza kuikumba sayari yetu ikiwa hatua zinazohitajika hazitachukuliwa.

Kitisho cha kuyayuka theluji ya kisiwa cha kaskazini ya dunia yetu-Groenland,wakaazi wa eneo la Afrika kati na maafa ya mazingira katika bonde la ziwa Tchad,maelfu ya wahanga wa dharuba ya Katrina huko New-Orleans,“mzozo wa wakimbizi wa kimazingira unatishia kugeuka janga kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa“ anaashiria Professor Norman Myers-wa chuo kikuu cha Oxford.

Pekee mwaka 2000,kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya msalaba Mwekundu,na Hilal Nyekundu, idadi ya wakimbizi wa kimazingira ilikua takriban sawa na ile ya wakimbizi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe-yaani karibu watu milioni 25…

Idadi hiyo inaweza kuongezeka mara dufu hadi mwaka 2010 na kufikia wakimbizi 100 milioni hadi mwisho wa karne hii,kutokana na kuzidi hali ya ujoto-anashadidia Prof.Meyers ,ambae ni mmojawapo wa wataalam waaliotunga ripoti hiyo .

„Watu watazidi kuyahama maeneo yao kwasababu ya hali ya hewa“,ameonya kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya taaluma ya Mazingira katika chuo kikuu cha Oxford-Thomas Downing.

Kuanzia Tuvalu kusini mwa bahari ya Pacifc,au Maladives katika bahari ya Hindi,kuzidi hali ya ujoto kwa degree tatu za Celcius na kuzidi mara dufu kiwango cha moshi wa sumu wa viwandani hadi mwisho wa karne hii,ni matukio yanayotisha kwa dunia yetu ripoti hiyo imesema.

Waasisi wa ripoti hiyo wanajaribu kuwagutua sio tuu wanasiasa na wanauchumi bali hata wananchi wa kawaida.

Martin Beniston,mtaalam wa hali ya hewa kutoka chuo kikuu cha geneva Uswisi ni miongoni mwa waasisi wa ripoti hiyo.Anahisi mwito wao utazingatiwa.

„ Nnahisi tangu mwaka mmoja au miwili hivi watu wameanza kutanabahi.Nnaamini hii ni mara ya kwanza katika kadhia hii kuona mmwamko kama huu na kutokana na mwamko huu wanaviwanda na wanasiasa wa nchi kubwa kubwa wanaweza kuzindukana na kupitisha hatua zinazohitajika.“

Hajakosea bwana martin Beniston.Kansela Angela Merkel ameshasema „ nishati na hifadhi ya hali ya hewa ni changamoto kubwa kabisa zinazowakabili walimwengu.Kansela Angela Merkel ametangaza wazi kabisa,suala la mabadiliko ya hali ya hewa ni moja wapo ya mada zinazopewa umuhimu mkubwa katika wadhifa wa Ujerumani kama mwenyekiti wa Umoja wa ulaya na jumuia ya mataifa tajiri kwa viwanda G-8 .