1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wajadili nishati na mabadiliko ya hali ya hewa

Mtullya, Abdu Said13 Machi 2008

Viongozi wa nchi na serikali wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kujadili usalama wa nishati na njia za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

https://p.dw.com/p/DNq9
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.Picha: AP


Viongozi wa nchi na serikali wa Umoja wa Ulaya leo wanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wao,mjini Brussels kujadili masuala ya usalama wa nishati, mabadiliko ya hali ya hewa na mageuzi katika nchi zao.

Viongozi hao kutoka nchi  27, kwenye mkutano wao pia watajadili suala la umoja wa nchi zinazopakana na bahari ya  Mediterania litakalowasilishwa kwa pamoja baina ya raisNicolas Sarkozy wa Ufaransa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.

Ujerumani  na Ufaransa  ziemeweka kandoa  tofauti zao juu ya suala hilo kufuatia mkutano wa viongozi wa  nchi hizo wa hivi karibuni.

Lakini awali ya yote mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya unaotarajiwa kuendelea hadi kesho utajadili masuala ya  usalama wa nishati na mabadiliko ya hali  ya hewa.

Nchi za Umoja huo zinaazimia kusimama   safu ya mbele katika juhudi za kupunguza  utoaji wa gesi zinazoathiri mazingira.

Viongozi kutoka nchi 27 za Ulaya watapokea  taarifa inayotahadharisha jinsi   amani ya dunia inavyohatarishwa. Taarifa hiyo pia inatabiri wimbi kubwa la wakimbizi kutoka barani Afrika na kutoka mashariki ya kati kuanzia mwaka wa 2010.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya kwenye mkutano wao pia watajadili namna ya kuelekeza  uhusiano wa  nchi zao na Serbia baada ya Kosovo kujitangazia uhuru hivi karibuni.