1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano kuhusu Somalia waanza London

Wawakilishi wa ngazi ya juu wa serikali 53 na mashirika ya kimataifa wanakutana mjini London, Uingereza kuzungumzia jinsi ya kuupa msukumo mchakato wa amani nchini Somalia.

Somalia's Prime Minister Mohamed Ali Abdiweli attends a news conference after meeting with European Commission President Jose Manuel Barroso at the Commision's Headquarters in Brussels February 21, 2012. REUTERS/Sebastien Pirlet (BELGIUM - Tags: POLITICS)

Wazrri Mkuu wa Somalia Mohamed Ali Abdiweli

Miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo ni katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-moon na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Hillary Clinton. Mwandishi wetu, Ludger Schadomsky, ambae yupo mjini London amesema mwenyeji wa mkutano huo ana masilahi yake.

Wakati unapita, Agusti mwaka huu unamalizika muda wa serikali ya mpito ya Somalia na hakuna katika jumuia ya kimataifa anaetaka kuona haali ya kutokuwepo uongozi ikitawala katika nchi hiyo iliyoathirika kwa njaa na kuzongwa na visa vya magaidi wanaofuata itikadi kali ya dini ya kiislam.Ngumi zilizozuka hivi karibuni bungeni nchini Somalia zimewafanya watu watanabahi iko mbali sana njia ya nchi hiyo muhimu kijeografia katika pembe ya Afrika kuelekea katika mfumo wa demokrasia ya magharibi.

Hata juhudi za kuifanyia marekebisho katiba,kazi inayowahusisha pia wanasheria wa Ujerumani, zinahitaji msukumo mpya.

Mwenyeji wa mkutano huo anafuata masilahi maalum.

Idadi kubwa ya vijana wa Kisomali wenye passpoti za Uingereza wanafunga safari hadi katika nchi hiyo ya pembe ya Afriika ili kujiunga na mapambano ya kigaidi.Ni kitisho kikubwa kwa usalama.Uingereza imepania kuhakikisha usalama wa nchi yake kwasababu ya michezo ya Olympic ya msimu wa kiangazi mwaka huu.

A young member of an Islamic militia group leads the way with other fighters as they patrol in southern Mogadishu ,Wednesday Aug. 19,2009. (AP Photo/Farah Abdi Warsameh)

Wanamgambo waasi nchini Somalia

Kwa hivyo haikuwa bahati nasibu pale waziri anaeshughulikia masuala ya Afrika Henry Bellingham alipoutembelea msikiti wa Finsbury Park kaskazini ya London,muda mfupi kabla ya mkutano huo kuitishwa.Kabla ya hapo waziri wa mambo ya nchi za nje William Hague aliutembelea kwa ghafla mji mkuu wa Somalia Mogadischu-ziara iliyopigiwa upatu sana na vyombo vya habari na kufungua upya ofisi ya ubalozi wa Uingereza.

Mada kuu mazungumzoni itahusiana bila ya shaka na tangazo lililotolewa mapema mwezi huu la kuungana wanamgambo wa kiislam wa Al Shabaab na mtandao wa kigaidi wa Al Qaida.Wajumbe mkutanoni watajaribu kusawizisha mwanya ulioko kati ya nchi za magharibi zinazojishughulisha na mzozo wa Somalia na mataifa ya kiarabu yanayowakilishwa na Qatar,Uturuki na Umoja wa Falme za kiarabu.Mataifa ya kiarabu yamekuwa yakilalamika dhidi ya msimamo wa Marekani na washirika wao katika eneo hilo-Ethiopia,wanaopinga moja kwa moja kufanyika mazungumzo pamoja na al Shabab.

Marekani na Uingereza hawataki kuzungumza na Al Shabaab.

Mdadisi wa masuala ya Somalia katika taasisi ya taaluma za usalama ISS mjini Nairobi Emmanuel Kisangani anasema Mmarekani na Uiengereza hawataki kuzungumza na Al Shabaab kwasababu bado wanawaangalia kuwa ni wafuasi wa kundi la magaidi.Wanahofia bwasije wakajipatia uhalali.

Anasema wale wanaounga mkono watu wazungumze na Al Shabab wana hoja zao pia nazo ni pamoja na ile hali kwamba Al Shabaab wanadhibiti sehemu kubwa ya Somalia na kwamba wananchi wengi wanathamini juhudi zao za kuimarisha usalama na kupambana na uhalifu.Emmanuel Kisangani anahisi ufumbuzi wa mzozo wa Somalia hauwezi kupatikana kwa mtutu wa bunduki.

Masilahi ya usalama yanatangulizwa mbele pia na ujumbe wa Ujerumani katika mazungumzo ya mjini London.Mwakilishi wa wizara ya mambo ya nchi za nje anaeshughulikia masuala ya Afrika Walter Lindner anazungumzia lengo la mkutano wa London na kusema "Lengo kusema mkweli ni kumalizika kipindi cha mpito msimu wa kiangazi,lakini pia kuhakikisha watu wanasonga mbele baada ya miaka 22 ya mkwamo. Maafa yaliyowasibu binaadam katika pembe ya Afrika yametugutuwa,lakini pia uharamia na ugaidi nchini humo pamoja na wakimbizi wanaoipa kisogo nchi hiyo yote hayo ni mamambo yanayotulazimisha tulishughulikie kwa makini zaidi suala hili na kwa namna hiyo nnaamini mkutano huo utatoa mchango wake".

Ujerumani linalisaidia baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika katika shughuli zake nchini SOmalia.Kwa kufungua hivi karibuni ofisi ya ubalozi nchini Djibuti,Ujerumani inataka kuchangia vyema zaidi katika juhudi za kuimarisaha utulivu katika eneo la pembe ya Afrika.

Mwandishi:Ludger Schadomsky(MM Regionen Afrika)/Hamidou Oummilkheir
Mhariri:Josephat Charo

DW inapendekeza

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com