Mkutano kati ya Olmert na Bush Washington | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 19.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mkutano kati ya Olmert na Bush Washington

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert yuko Washington na anatazamiwa leo kukutana na rais Bush huko Ikulu.

Waziri mkuu mpya wa Palestina

Waziri mkuu mpya wa Palestina

Baraza la makanisa ulimwenguni-World Council of Churches-lenye makamo yake mjini Geneva nalo lilitangaza jana kuanzisha kampeni ulimwenguni kote ya kuishinikiza Israel kumaliza kuzikalia kwake ardhi za waarabu ilizoziteka katika vita vya 1967.

Mkutano kati ya rais George Bush na waziri mkuu wa Israel unafuatia wiki ya machafuko katika ardhi za wapalestina pamoja na chama cha HAMAS kuudhibiti mwambao mzima wa Gaza na rais Mahmud Abbas kukitimua chama cha Hamas katika serikali ya muungano ilioundwa hapo machi.

Hatua ya rais Abbas ya kuiteua serikali mpya isioingiza chama cha Hamas ilifungua njia ya kurejeshwa kwa misaada ya moja kwa moja ya kimataifa kwa serikali hiyo mpya ya Palestina ambayo hapo kabla ilizuwiliwa na Marekani na washirika wake wa Umoja wa ulaya kwa zaidi ya mwaka.

Muda mfupi kabla ya ziara ya waziri mkuu Olmert huko White House,mabingwa wa mashariki ya kati kama vile Robert Malley, kutoka kikundi cha kukabiliana na misukosuko “Int.Crisis Group” walitoa ila kali kwa sera za rais Bush huko Mashariki ya kati.Malley asema:

“Miaka 5 iliopita rais Bush alipendekeza mfumo wa dola 2 huko:yaani Israel na Palestina.Kutimilia kwa shauri hilo hakuonekani.Pia ni dhahiri-shahiri kwamba jaribio la kukidhofisha chama cha Hamas na ikimkinika kukitimua haraka nje ya serikali ya Palestina kumeshindwa kabisa.”

Badala ya kuangalia mbele kwa matumaini mkutano kati ya Bush na Olmert hii leo huko Washington una shabaha ya kupunguza tu dhara.Mkakati wa Marekani ni wazi kabisa: Msaidie rais Mahmud Abbas na serikali yake ya dharura huko Ukingo wa magharibi na itenge Hamas katika mwambao wa gaza mbali sana kama iwezekanavyo bila huko kuzuka msiba wa kibinadamu.

Waziri wa nje wa Marekani dr.Condoleeza Rice asema:

“Tuna azma ya kuondoa vikwazo vya kiuchumi tulivyoiwekea serikali hii, kwavile hapo kabla ilifunga mapatano na Israel na ikipinga matumizi ya nguvu.”

Katika kulenga shabaha hii, yabainika Marekani inategemea ushirikiano wa Israel.Risala ya waziri wa nje Dr.Rice ingawa imeelezwa kirafiki,kimsingi lakini ni wazi kabisa na si ya kigeugeu.Hakuwezi kuwapo shabaha nyengine mbali na kuwa na Palestina moja ambayo itaishi kwa salama na amani na Israel.

“Waisraeli wapaswa kujua jambo moja.Dola la Pelestina likiundwa ,litachangia usalama zaidi Mashariki ya kati na sio kila mara vitendo vipya vya kigaidi vinatokea.”

Huko Geneva,Uswisi,Baraza kuu la makanisa ulimwenguni limetangaza jana kwamba linapanga kuanzisha kampeni kote duniani kuyataka makanisa kuishinikiza Israel ihame kutoka ardhi za warabu ilizozikalia tangu Juni,1967.

Likiwa limeasisiwa 1948,Baraza hilo la makanisa duniani linapalilia umoja wa wakristu.Linajumuisha makanisa 347 ya kiprotestanti,kiorthodox,Anglican na mengineo yakiwakilisha kwa jumla hadi wakristu milioni 560 katika nchi zaidi ya 110.

Nae mfalme Abdullah wa Saudia Arabia ,mcheza-karata muhimu katika siasa za Mashariki ya kati alisema jana kuwa ugomvi katika ardhi za wapalestina,Lebanon na Iraq, waweza ukaingiza dunia nzima na hivyo Saudi Arabia inafanya juhudi kubwa kuifikia amani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com