Mji wa Sirte bado umezingirwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.10.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mji wa Sirte bado umezingirwa

Mji wa Sirte nchini Libya, mahali alikozaliwa kiongozi aliyeondolewa madarakani Muammar Gaddafi unaendelea kuzingirwa na majeshi yanayounga mkono baraza la mpito la taifa.

default

raia wakishangiria wakati majeshi ya mapinduzi yalipopata udhibiti wa bandari ya mji wa Sirte.

Mji wa Sirte nchini Libya , mahali anakotoka kiongozi aliyeondolewa madarakani Muammar Gaddafi unaendelea kuzingirwa. Siku ya Ijumaa, majeshi ya baraza la mpito yametoa kwa wakaazi wa mji huo, siku mbili kuondoka mjini humo, licha ya kwamba wametoa muda kama huo mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni.

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu , ambalo wafanyakazi wake wameanza kupeleka madawa katika mji huo, wameliambia shirika la habari la AFP kuwa hali ndani ya mji wa Sirte ni mbaya. Mji huo umezingirwa kwa wiki kadha na majeshi yanayoliunga mkono baraza la taifa la mpito. Mkuu wa baraza hilo, Mustafa Abdel Jalil amesema kuwa wapiganaji wake wanadhibiti maeneo kiasi ya kilomita tano kutoka katikati ya mji huo, lakini wanakabiliana na upinzani mkubwa kutoka majeshi tiifu kwa Muammar Gaddafi.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com