1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MINUSMA waanza kuondoka Mali

Josephat Charo
17 Oktoba 2023

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali wametangaza kuanza kuondoka kutoka kambi zao mbili za Tessalit na Aguelhok katika eneo la Kidal.

https://p.dw.com/p/4XcWa
Mali | MINUSMA Mission der Vereinten Nationen
Mmoja ya wanajeshi wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA).Picha: Nicolas Remene/Le Pictorium/MAXPPP/dpa/picture alliance

Hatua inayoanzisha awamu mpya ya kulazimishwa kuondoka ambayo inaibua hofu kwamba mapigano yataongezeka kati ya wanajeshi wa Mali na makundi yenye silaha.

Soma zaidi: Watu 64 wauawa nchini Mali katika mashambulizi mawili tofauti

Kikosi hicho cha amani cha Umoja wa Matiafa kinachofahamika kama MINUSMA kilitarajiwa kuondoka kutoka kambi zake katikati ya Oktoba lakini kikaahirisha wakati eneo hilo lililopokabiliwa na ongezeko la machafuko na mapigano.

Soma zaidi: Awamu ya pili ya kuwaondoa walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali "itakuwa ngumu"

Kwa mujibu wa maafisa wawili wa uwanja wa ndege, jeshi la Mali limetuma ndege mbili katika kambi ya Tessalit zikiwabeba vikosi vya wanajeshi na wapiganaji wa kundi la mamluki la Wagner kutoka Urusi.