1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka minane tangu kufariki dunia Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania

15 Oktoba 2007

Oktoba 14, miaka minane iliopita, rais wa kwanza wa Tanzania na baba wa taifa hilo, Mwalimu Julius Nyerere, alifariki dunia katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas, mjini London, Uengereza.Yeye alikuwa miongoni mwa viongozi wa Kiafrika walioshiriki moja kwa moja katika vita vya ukombozi vya nchi zao na pale nchi hizo kuwa huru wakakamata usukani na kuamua njnia gani nchi hizo zielekee.

https://p.dw.com/p/C7hk
Maandamano na mlolongo wa maelfu kwa maelfu ya watu katika mazishi ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere
Maandamano na mlolongo wa maelfu kwa maelfu ya watu katika mazishi ya Hayati Mwalimu Julius NyererePicha: AP

Licha ya kwamba mafundisho ya marehemu Julius Nyerere juu ya siasa ya ujamaa na kujitegemea sasa hayatekelezwi, kinyume na ilivokuwa pale alipokuwa madarakani, hata hivyo Watanzania wanapobishana katika masuala mbali mbali hurejea nyuma na kumkumbuka Mwalimu Nyerere kama kituo cha uadilifu, na hasa ile ndoto isiotimia bado ya kuwatupia jicho la huruma watu wa tabaka la chini.

Ni Othman Miraji wapendwa wasikilizaji katika makala haya ya DARUBINI, uchambuzi wa kisiasa wa kila wiki kutoka Radio Deutsche Welle, mjini Bonn, Ujerumani.

Hebu kwanza tuyadurusu matamshi ya Mwalimu Nyerere tuliyoyapata katika maktaba yetu. Akizungumzia juu ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, jaribio ambalo wachunguzi wanasema lilikuwa na nia nzuri , lakini lilishindwa kuleta matarajio yaliowekewa:

Insert: Nyerere 1 Ujamaa na Kujitegemea

Mwalimu anasifiwa kuwa muasisi wa Muungano wa Tanganyika na Visiwa vya Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alikuwa mkakamavu juu ya muungano huo na kuyapuunza matakwa ya baadhi ya watu waliotaka ipigwe kura ya maoni kuwauliza watu wa sehemu mbili za Muungano kama wanaukubali…

Insert:: Nyerere 2 Muungano wa Tanzania…

Hayati Mwalimu Nyerere pumzi zake pia alizielekeza kutaka Bara la Afrika liwe na Umoja, mfano wa Umoja wa Ulaya ulimvutia…

Insert: Nyerere 3 Umoja wa Afrika….

Kuyajua zaidi yale yaliofanywa na Hayati Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake, mwandishi wetu wa Dar es Salaam, Hawra Shamte, ameandaa yafuatayo:

Insert: Mwalimu Revisited

Na kwa hayo kutoka kwa mwandishi wetu wa Dar es Salaam, Hawra Shamte, aliyeukumbuka mwaka wa nane tangu muasisi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Nyerere, kufariki, tunakamilisha makala haya ya DARUBINI, uchambuzi wa kisiasa wa kila wiki kutoka Radio Deutche Welle, Bonn, Ujerumani. Hadi mara nyingine…