1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 23 ya kuungana tena kwa Ujerumani

Admin.WagnerD3 Oktoba 2013

Miaka 23 baada ya kuungana tena kwa Ujeurmani mbili, mabadiliko yanaonekana katika upande wa Ujerumani mashariki. Miundombinu imekuwa bora ikilinganishwa na magharibi, lakini tofauti za kiuchumi bado zingalipo.

https://p.dw.com/p/19tBL
Raia wakiwa wamejichora katika rangi za bendera ya taifa ya Ujerumani. Sherehe za kitaifa za kumbukumbu ya miaka 23 ya kuungana tena kwa Ujerumani magharibi na mashariki zinafanyika katika jimbo la Baden-Württenberg, kusini mwa Ujerumani.
Raia wakiwa wamejichora katika rangi za bendera ya taifa ya Ujerumani. Sherehe za kitaifa za kumbukumbu ya miaka 23 ya kuungana tena kwa Ujerumani magharibi na mashariki zinafanyika katika jimbo la Baden-Württenberg, kusini mwa Ujerumani.Picha: picture-alliance/dpa

Kansela Helmut Kohl, ambaye aliesherekea kuungana tena Ujerumani mbili kwa mara ya kwanza, aliwahi kuwaahidi wakaazi wa majimbo sita ya Ujerumani mashariki mandhari ya kupendeza. Lakini katika miaka ya kwanza ya muungano huo, hali ilikuwa kinyume cha hivyo. Miundombinu chakavu, kufilisika kwa makampuni, viwango vya juu vya ukosefu wa ajira na kuhama kwa vijana kwa wingi, kiasi kwamba baadhi ya maeneo yalitishiwa kubaki matupu. Hivi sasa ni miaka 23 tangu Ujerumani mbili ziungane tena. Je, kuna lililotimia katika ahadi ya Kohl?

"Mandahari hayo kwa sasa yamefikiwa kwa sehemu fulani, kiwango cha ukosefu wa ajira kimeshuka, miundo mbinu imeboreka, na hali ya makampuni siyo mbaya sana ilikinganishwa na upande wa magharibi. Hiyo inamaanisha kuwa karibu ujenzi wa magharibi umekamilika," ansema Klaus Heiner Röhl mtaalamu kutoka Taasisi ya uchumi ya Ujerumani ya mjini Koloni.

Uwekezaji waongezeka mashariki
Mwezi Septemba asilimia 9.6 ya wakaazi wa Ujermani mashariki ndiyo walikuwa hawana ajira, wakati kiwango cha ukosefu wa ajira katika Ujermani magharibi kilikuwa asilimia 6.6. Miaka michache iliyopita, kiwango cha ukosefu wa ajira katika upande wa mashariki kilikuwa mara mbili ya ilivyokuwa katika Ujerumani magharibi. Mtu ambaye amekuwepo Ujerumani mashariki hivi karibuni, hashangai vibaya kuhusu miundombinu mipya, ila tu baadhi ya manisapaa za upande wa magharibi zinaweza kuona wivu.

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck na bibi yake Daniela Schadt, rais wa bunge la Ujerumani Norbert Lammert, Kansela Angele Merkel na waziri mkuu wa jimbo la Baden-Württenberg, Winfried Kretschmann, wakiwa katika ibada ya kusherehekea miaka 23 ya kuungana upya kwa Ujerumani mbili.
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck na bibi yake Daniela Schadt, rais wa bunge la Ujerumani Norbert Lammert, Kansela Angele Merkel na waziri mkuu wa jimbo la Baden-Württenberg, Winfried Kretschmann, wakiwa katika ibada ya kumbukumbu ya miaka 23 ya kuungana upya kwa Ujerumani mbili.Picha: picture-alliance/dpa

Yapo makampuni machache ya Ujerumani mashariki ambayo yamefanikiwa kufikia kiwango cha kimataifa, yakiwemo yale ya zamani kama vile Carl Zeiss na Jenoptik, lakini pia yamo makampuni yaliyoanzishwa baada ya mabadiliko, kama ile inayotengeneza zana ya Roth & Rau, na ile ya kuuza magari ya Mitec Group, bila kusahau uwekezaji mkubwa wa makampuni ya magari kama vile Volks Wagen, BMW au Daimler mashariki mwa Ujerumani.

Pia sekta ya umeme wa jua na nishati ya nguvu ya upeno ni miongoni mwa vitega uchumi vyenye ufanisi mashariki mwa Ujerumani. Mafanikio haya yamesaidia kupunguza uhamaji wa nguvukazi, na jimbo la Saxony lililoko mashariki mwa Ujerumani linafurahia kupokea wahamiaji, anasema Röhl na kuongeza kuwa kwa sasa ujenzi mpya wa Ujerumani mashariki umekuwa hadithi ya mafanikio.

Tofauti za kimapato
Kulingana na uchunguzi wake, tija ya kiuchumi katika majimbo mapya Ujeruman ingali bado inafikia thuluthi mbili ya kiwango cha magharibi.Kwa maneno mengine, mkaazi wa Ujerumani mashariki anafikia thuluthi mbili tu ya pato la mkaazi wa Ujerumani magharibi.Pengo, kwa mujibu wa Klaus-Heiner Röhl linatokana na tofauti iliyopo katika miundo mbinu.

"Tofauti kubwa zaidi ni ukosefu wa makampuni makubwa makubwa, mashirika, benki na mashirika ya bima.Yote hayo ni mashirika yanayoweza kutoa tija kubwa.Yote hayo yana makao yao msakuu Ujerumani Magharibi."

Kuna uwezekano mdogo kwa hali hii pia kubadilika kwa sababu, "…kwa nini kampuni ya Siemens ihame kutoka Munich au Deutsche Bank iondoke kutoka Frankfurt?", anauliza Klaus Röhl.

Sherehe za siku ya Muungano zilianza kufanyika mjini Stuttgart, jimboni Baden-Württenberg.
Sherehe za siku ya Muungano zilianza kufanyika mjini Stuttgart, jimboni Baden-Württenberg.Picha: picture-alliance/dpa

Magharibi yainufaisha mashariki
Licha ya kufanya vizuri kiuchumi, kuna pengo kubwa katika mishahara. Wafanyakazi wa magharibi wanapata asilimia 80 tu ya viwango vinavyotolewa magaharibi, lakini Röhl anasema kwa mujibu wa utafiti mpya viwango hivyo vinafikia asilimia 97 ya upande wa magharibi hivi sasa, hii ikitokana kwa kiasi kikubwa na uhamishaji wa fedha kwa sekta ya umma mashariki mwa Ujerumani.

Kwa ujumla, fedha zilizohamishwa kutoka magharibi kwenda mashariki hadi sasa zinafikia euro trilioni mbili. Kulingana na makubaliano ya sasa, malipo hayo yataendelea hadi mwaka 2019, na baada ya hapo upande wa mashriki utakuwa sawa na ule wa magharibi kifedha.

Mwandishi: Zhang Danhong
Tasfiri: Iddi Ismail Ssessanga
Mhariri: Saum Yusuf