1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia ziarani Ujerumani

8 Novemba 2007

Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia amepokewa kwa heshima ya kijeshi alipowasili Berlin,mji mkuu wa Ujerumani kwa ziara ya siku tatu.

https://p.dw.com/p/C778
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel akimpokea Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia,mjini Berlin
Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel akimpokea Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia,mjini BerlinPicha: AP

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali mjini Berlin,Mfalme Abdullah na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wamejadili maendeleo ya mazungumzo kati ya Israel na Wapalestina kabla ya mkutano wa amani wa Mashariki ya Kati.Mkutano huo unatazamiwa kufanywa baadae mwezi huu nchini Marekani.

Mada zingine zilizojadiliwa na viongozi hao wawili zimehusika na jinsi matokeo ya nchini Iran yanavyoathiri ulimwengu wa Kiislamu pamoja na utulivu nchini Afghanistan na Pakistan.Hii leo Mfalme Abdullah atapokewa na meya wa jiji la Berlin,Klaus Wowerweit.

Mfalme Abdullah alie na umri wa miaka 84,alianza ziara yake ya barani Ulaya nchini Uingereza.Siku ya Ijumaa ataelekea Uturuki.