MESENBERG: Merkel akutana na Chirac
23 Februari 2007Matangazo
Rais wa Ufaransa Jacques Chirac na kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel wamekutana leo mjini Mesenberg kaskazini mwa Berlin katika mkutano wa kilele ambao hufanyika baina yao mara kwa mara.
Mkutano huo ulizungumzia kwa kina mpango wa kuifanyia mageuzi kampuni ya ndege ya Airbus. Maelfu ya nafasi za ajira zinatarajiwa kupotea nchini Ujerumani na Ufaransa huku kampuni ya EADS ikijiandaa kutekeleza mpango wa kupunguza matumizi kwa kiasi cha euro milioni tano katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Maafisa wa Ujerumani na Ufaransa wamekuwa wakizozana juu ya wapi nafasi za ajira zipunguzwe. Merkel na Chirac wamekubaliana kuisaidia kampuni ya EADS.