Mawaziri wa usafiri wa Umoja wa Ulaya wafanya mkutano
20 Aprili 2010Matangazo
Mawaziri wa usafiri wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kufungua sehemu ya anga iliyokuwa imefungwa kutokana na wingu la majivu yaliyosababishwa na mripuko wa volkano nchini Iceland.
Hatua hiyo imefikiwa katika mkutano wao wa dharura walioufanya jana kwa njia ya video. Waziri wa Usafiri wa Ujerumani, Peter Ramsauer alisema kuwa ndege zitaanza kurejea katika hali ya kawaida kuanzia leo, ingawa itakuwa kulingana tu na masharti makali ya usalama.
Maelfu ya wasafiri wameendelea kukwama kufuatia kufungwa kwa anga za maeneo mengi ya Ulaya kwa siku ya tano mfululizo. Mashirika ya ndege yamesema yamepata hasara ya zaidi ya euro milioni 740. Anga ya Ujerumani itaendelea kufungwa hadi angalau mchana wa leo.