1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya Magharibi yaishtumu Urusi

27 Agosti 2008

Mataifa karibu yote ya Ulaya yameonyesha upinzani wao kwa hatua ya Urusi kuyatambua majimbo ya Abkhazia na Ossetia ya kusini kujitangazia uhuru.

https://p.dw.com/p/F5kK
Rais wa Urusi Dmitry Medvedev akitangaza amri ya kuyatambua majimbo ya Abkhazia na Ossetia ya kusiniPicha: AP

Baada ya rais wa Urusi Dmitry Medvedev jana Jumanne kutambua uhuru wa majimbo ya Georgia yanayotaka kujitenga ya Abkhazia na Ossetia ya kusini , mataifa karibu yote ya magharibi yameeleza kutokukubaliana kabisa na uamuzi huo. Serikali ya Marekani nayo haraka imeeleza kutoridhishwa kwa na maamuzi hayo.

Hii inaonyesha vipi siasa za Urusi zilivyo: Watatia saini makubaliano na siku ya pili watayavunja. Watatia saini makubaliano ya umoja wa mataifa na baada ya muda mfupi hawayajali tena. Anasema Tony Fratto, msemaji wa rais George Bush wa Marekani mjini Washington.

Katika mkataba wa kusitisha mapigano uliopatanishwa kwa msaada wa Ufaransa Urusi ilikubaliana kabisa na umoja wa majimbo hayo ya Georgia. Pamoja na maazimio yote ya umoja wa mataifa juu ya Georgia.

Lakini ghafla Urusi hivi sasa haitaki tena kutoyatambua kabisa masharti haya.

Kwa kufanya hivyo inahatarisha nafasi yake katika dunia, kama anavyosema msemaji wa rais George Bush, mjini Washington Tony Fratto.

Urusi kwa hiyo imejifungia njia zote kuingia katika umoja wa mataifa kutokana na hali hii.

Marekani ambayo ina kura ya turufu itajaribu kuzuwia juhudi zote za Urusi katika baraza la usalama la umoja wa mataifa, kutaka majimbo ya Abkhazia na Ossetia ya kusini yatambuliwe kuwa huru.

Serikali ya Marekani inaangalia hata hivyo uwezekano wa kuweza kulishughulikia kwa njia sahihi suala hili la Urusi. Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani inafikiria kusitisha makubaliano ya kinuklia baina ya Urusi na nchi hiyo.

Makubaliano hayo yalitiwa saini baina ya rais George Bush na Putin, kuhusiana na matumizi ya pamoja ya amani ya nishati ya kinuklia. Na kutokana na hayo ni muhimu hivi sasa kuisaidia Georgia, amesisitiza msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani.

Lakini kwa upande wa wanasiasa mjini Brussels hatua ya rais wa Urusi kuyatambua majimbo hayo mawili yanayotaka kujitenga nchini Georgia kuwa ni huru haijawashangaza. Kwa muda wa mwezi mmoja hivi hali hiyo ilionekana wazi, pia ni kulipiza kisasi kutokana na mzozo wa jimbo la Kosovo kutoka Serbia. Wakati huo mataifa mengi ya umoja wa Ulaya yalilitambua taifa jipya la Kosovo. Urusi ilishutumu sana kitendo hicho.

Hata hivyo umoja wa Ulaya unatenganisha kabisa masuala haya mawili na hali katika eneo la Causasus. Kwamba suala la Kosovo linahusika na kuvunjika kwa jamhuri ya Yugoslavia , ambapo mambo hayo hayafanani.

Msisitizo huu kuhusiana na kuwa na Georgia moja , una maana kuwa umoja wa Ulaya unataka kuliangalia suala la kuwa Urusi inakiuka haki za binadamu. Hata hivyo msemaji wa tume ya Ulaya amesisitiza kuchukua tahadhari kuhusu matumizi ya maneno dhidi ya Urusi.