1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na hujuma ya Septemba 11-2001

11 Septemba 2007

Ulimwengu mzima unakumbuka siku ya leo -miaka 6 iliopita pale jengo kuu la biashara la New York -maarufu World Trade Center na Pentagon mjini Washington yaliporipuliwa kwa mastumizi ya ndege.

https://p.dw.com/p/CB1N
Ndege ilipojigonga juu ya jengo moja sio WTC.
Ndege ilipojigonga juu ya jengo moja sio WTC.Picha: AP

Leo, miaka 6 kamili iliopita ,ilifanyika ile hujuma iliopata umaarufu ‚Septemba 11’.Minara 2 ya jengo mashuhuri la biashara mjini New York-World Trade Centre iliporomoka.Maalfu ya wanadamu waliuwawa.Shambulio lile la Septemba 11, likabadili sura ya dunia nzima na ulioathirika mno zaidi ni mji wa New York.

Hali ikoje leo, miaka 6 baadae ?

Hali ya wasi wasi ingali imetanda katika jiji la New York na hasa katika njia za reli za chini kwa chini.Kuna ilaani zisemazo:Ukigundua kitu cha shaka shaka,sema.“

Hali hii imebakia hivyo miaka 6 tokea shambulio lile la Septemba 11, 2001.

Kwa kawaida maisha yamerudi kuwa kawaida-bussiness as usual-kama wasemavyo.L akini, mara tu pakigunduliwa kitu kisicho cha kawaida,wasi wasi huzagaa na hofu hutanda,kwani kila mmoja anakumbuka jiinamizi la Septemba 11.

Ilipotokea kitu cha kutia shaka shaka karibuni ilikuaje ?

„Baadhi ya watu waliingiwa na kihoro,waliangua vilio na kila mmoja akidhani limezuka balaa jingine la Septemba 11.“

Hivo ndivyo shahidi mmoja alivyosimulia wasi wasi na hofu majiani pale bomba la mvuke liliporipuka mjini New York,Julai mwaka huu.

Wingu kubwa la mvuke lilipaa hewani kutoka jengo la Grand Central na kutoa picha la kuporomoka sawa na zile za kustusha za jengo la World Trade Centre.

Jazba zikapanda tena kama anavyosimulia mtaalamu wa saikolojia Sylvia Berklein:

„Nadhani wakaazi wa New York ukiwalinganisha na wa sehemu nyengine,tayari wamekomaa katika uvumilivu.Nadhani,wamejaribu kurejea maisha ya kawaida,hatahivyo mkasa ule unabaki vichwani mwao na hauwezi kusahaulika haraka hivyo.“

Wakaazi wa jiji la NY wameingiwa na wasi wasi na ukitupa jicho la kwanza kuwaangalia hugundui wasi wasi huo.Kwani, katika jiji hili la wakaazi milioni 8,hakuna ataeweza kuishi ikiwa anaishi na woga kila siku kwamba kutaripuka tena.

Hatahivyo, watu wanajkodoa macho barabara.Kuna bado makarani ambao afisini mwao wanafungua barua wanazopokea wakiwa wamevaa glovu kujikinga na miripuko.

Ukaguzi wa hali ya usalama katika njia za reli za chini ya ardhi huimarishwa mara tu shaka-shaka ndogo tu ikizuka.Uchunguzi umeonesha kuwa kila mmoja anaitikia tofauti juu ya hali kama hii.Kuna baadhi ya watu wameshaota ngozi ngumu kuna wengine jambo dogo tu lawakumbusha kisa cha Septemba 11.Kuna wale wanaosema ah, tumzowea hayo.

Hatahivyo, suala moja ambalo haiepukiki kwa diwani mkuu wa jiji la NY Bloomberg ni kujibu panapozuka mripuko ghafula:Je, ni bomba la gesi au ndege ndogo iliojigonga kutokana na hitilafu ya kiufundi na imepaa juu ya anga la jumba fulani au ni shambulio la kigaidi ?

Diwani Bloomberg- jibu lake la kwanza-„Hakuna taarifa ya kitendo cha kigaidi.“