Maoni kuhusu Mjadala baina ya Angela Merkel na Frank-Walter Steinmeier
14 Septemba 2009Matangazo
Zikiwa zimebakia takriban siku 13 kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu, wagombea wawili wa kiti cha Ukansela, Angela Merkel wa chama cha CDU na Frank-Walter Steinmeier wa chama cha SPD jana usiku walishindana katika mjadala kwa njia ya televisheni kubainisha nani ana hoja nzito kuliko mwenzake. Hivi punde nimezungumza na Bibi Hannelore Steer, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Radio Berlin, Brandenburg. Grace Kabogo alianza kwa kumuuliza mtazamo wake kuhusu wagombea hao baada ya kuuangalia mjadala huo jana usiku.