1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makahama ya The Hague kuanza kusikiliza kesi za uahlifu wa Darfur

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXEh

THE HAGUE.Mahakama UN ya uhalifu ya mjini The Hague Uholanzi kuanzia mwakani, inatarajia kuanza kusikiliza kesi mbili, za uhalifu uliyofanywa dhidi ya wafanyakazi wa misaada ya kibinaadamu na askari wa kulinda amani huko Darfur nchini Sudan.

Ripoti iliyotolewa na kitengo cha haki za binadamu cha Umoja wa Mataifa iliishutumu Serikali ya Sudan kwa kushindwa kuwalinda raia kama inavyotakuwa na sheria za kimataifa.

Ripoti hiyo imesema kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita, majeshi ya serikali pamoja na wanamgambo wanaowaunga mkono wa Janjaweed yamewaua mamia ya raia.

Wakati huo huo kundi la wazee wenye heshima wa kimataifa, linalowajumuisha Askofu Desmond Tutu na Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter limetaka kusitishwa haraka kwa mapigano huko Darfur.

Kundi hilo limetaka kupelekwa haraka kwa jeshi la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur ili kuokoa maisha ya watu na kuongeza kuwa majaaliwa ya Dafur na kwa ujumla Sudan yote yako katika hali mbaya.