1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi ya Gadhafi yanasonga mbele dhidi ya waasi

30 Machi 2011

Nchini Libya kwenyewe wanajeshi watiifu kwa Kiongozi wa Libya,Muammar Gaddafi leo hii wamewarudisha nyuma waasi kutoka pembezoni mwa mji wa Sirte alikozaliwa kiongozi huyo .

https://p.dw.com/p/10k8A
Waasi nchini LibyaPicha: AP

Kwa upande mwengine ndege za kivita za muungano wa kimataifa zikiendelea na mashambulizi ya anga katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo. Duru kutoka katika uwanja wa mapambano zinaeleza kwamba,vikosi vya Gaddafi hivi sasa vinakaribia mji wenye hazina ya mafuta wa Ras Lanuf,ambao upo umbali wa kilometa 370 magharibi mwa makao makuu ya waasi huko Benghazi.

Waasi wenye silaha, ambao hawana ujuzi wowote wa kijeshi waliusogelea mji wa Sirte kwa umbali wa kilometa 100, kabla ya kukutana na kipingamizi kutoka kwa vikosi vya Gaddafi.

Krieg in Libyen
Vikosi vinavyomuunga mkono GaddafiPicha: AP

Waasi walianza kusonga mbele machi 19,baada Uingereza,Marekani na Ufaransa kuanza operesheni ya kuzuia ndege kuruka nchini Libya,ikiwa utekelezaji wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Tangu kuanza kwa operesheni hiyo ndege za kivita za vikosi vya Muungano zimekuwa zikishambulia kambi za jeshi, magari ya mzinga pamoja na vifaru nchini humo.

Akizungumza muda mfupi baada ya kurudishwa nyuma mpaka eneo la Bin Jawad,mpiganaji muasi,Ramadhan Berki alisema "imetupasa turudi nyuma haraka,ilikuwa hatari sana.Lakini kama ndege za Ufaransa zikirejea tena,leo hii jioni tutaingia Sirte na Tripoli baada ya siku tatu"

Berki alisema wanahitaji msaada kutoka kwa Ufaransa na Uingereza kwa kudai, bila mashambulizi yao ya anga Gaddafi atawaua.Amesema wanazo silaha lakini hazitoshi. Naye Msemaji wa Baraza la Mpito la Waasi,Mustafa Ghuriani amekanusha taarifa zilizoeleza kwamba Ufaransa na Marekani zinawapa silaha , akisema hao ni marafiki tu,wanaounga mkono jitihada zao.

Miripuko mingine mingi tofauti kutokana na hujuma za mabomu za ndege za kivita za majeshi ya muungano, imesikika mapema leo katika mji mkuu wa Libya - Tripoli karibu na makazi ya Gaddafi na kambi ya jeshi ya Tajura nayo imeripuliwa. Umoja wa kujihami wa NATO pia umekanusha taarifa za kuendesha operesheni za pamoja na Waasi nchini Libya au hata kuwapa silaha waasi hao.

Kamanda wa NATO,Admiral James Stavrids amesema kinachofanyika kutafuta hali halisi ya waasi katika wakati huu ambapo kumebainika uwezekano wa kuwepo wa kikundi cha waasi cha Al-Qaeda kilichojitumbukiza katika machafuko hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza alizungumzia pia swala hilo akisema"Tunavyoelewa maazimio ya Umoja wa Mataifa ni kwamba marufuku ya matumizi ya silaha ni kwa Walibya wote,ingawa inawaezekana silaha kupewa raia kwa ajili ya kujilinda,kwa mazingira fulani na masharti fulani ingawa hatujachukua hatua hiyo".

Krieg in Libyen Flash-Galerie
Mashambulizi ya anga ya majeshi ya MuunganoPicha: AP

Katika mji wa tatu kwa ukubwa wa Misrata,vikosi vya Gaddafi vimeingia katika ya mji kwa kishindo leo hii huku vikifyatua mizinga hewani ikiwa kama ishara ya kuudhibiti mji huo wa tatu kwa ukubwa nchini Libya. Akizungumzia hali ilivyo katika mji huo uliyopo kilometa, 214 mashariki mwa Tripoli,Msemaji wa waasi ameonya kwamba uwenda kukatokea mauji ya haraiki.

Taarifa kutoka mjini Misrata zinasema zaidi ya watu 142 wameuwawa na wengine 1400 kujeruhiwa tangu kuanza kwa machafuko nchini Libya machi 18 mwaka huu.

Mwandishi: Sudi Mnette//AFP

Mhariri: Abdul-Rahman