Mahujaj na mtandao wa Internet | Masuala ya Jamii | DW | 04.11.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Mahujaj na mtandao wa Internet

Mawasiliano ya kimambo leo,yanapendwa na mahujaj mwaka huu.Lakini sio wao tu, hata maafisa wa serikali wa Saud Arabia wanatumia Facebook na Twitter.

default

Waumini wa dini ya kiislam wanazunguka Al Qaaba,wakiwa katika ibada ya kutekeleza nguzo ya tano ya dini yao-Hajj

Mahujaj wanapokuwa Makka wanalizunguka al-Qaaba, mara nyingi marafiki zao nyumbani wanakuwa wanafuatilizia ibada hiyo kupitia mitandao ya kijamii. Kupitia mawasiliano ya kijamii, wanawasiliana na ulimwengu mzima na kuzungumzia hisia halisi walizo nazo wakati huu wanapokamilisha Hajj. Au wanatumia simu zao za Smartphone ili kujipatia maelezo kuhusiana na taratibu za Hijja, kujuana na mahujaji wengine au kuwasiliana kwa bei rahisi na familia zao nyumbani. Hata maafisa wa Saud Arabia wanatumia njia hizo mpya za mawasiliano ili kuwasaidia na kuwaongoza mahujaji. Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, mahujaji wanajipatia maelezo kuhusu makaazi na pia wasimamizi. Kwa hivyo, hakuna shaka yoyote kwamba njia mpya za mawasiliano zinakamata nafasi ya mbele pia katika ibada kubwa kubwa za kidini ulimwenguni, mfano wa hii ya Hajj.

Hujaji mmoja kijana anautumia mtandao wa kijamii wa Twitter kutekeleza mojawapo ya majukumu yake ya kidini: Anawaomba marafiki zake wanaoutumia pia mtandao huo wa kijamii wa Twitter, wasameheyane endapo aliwahi kumkosa mmoja kati yao. Anaendelea kuandika: "Kesho nnakwenda katika mji mtakatifu wa Makka, nisameheni ikiwa niliwahi kumkosa yeyote kati yenu": (Akiwa muislam, ili kumuomba Mungu amsamehe madhambi yote aliyoyafanya na Ili kukubaliwa maombi yake ,anabidi awaombe radhi wote wale ambao aliwahi pengine siku moja kuwatendeya maovu). Mtandao wa kijamii wa Twitter ndio njia bora anaoyiona ili kuweza kuwasiliana na wote wale ambao kabla ya kuja kuhiji hajawahi kuwaona au kuzungumjza nao kwa simu.

Hadsch 2009 Galerie

Mahujaj

Mitandao ya kijamii sio tu inawasaidia mahujaji wakati wa kujiandaa kuja kuhiji- bali pia kuhusu taratibu za Hijja wanapokuwa wameshawasili Makka. Baadhi ya mahujaj wanaelezea hisia zao kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook wanapokuwa wanaendeleza ibada yao: "Assalam Aleykum, hivi sasa niko katika mji mtakatifu wa Makka. Awali niliizunguka al-Qaaba- si hisia ambazo mtu anaweza kuzisimulia" ameandika haji mmoja kwa lugha ya kiarabu.

Baadhi ya mahujaji wananasa matukio ya ajabu ajabu au watu wa kuvutia, kwa njia ya video kupitiaYou Tube.

Hujaji mmoja ameandika kuhusu mtazamo wake wa kisiasa na kiuchumi kuhusiana na Hajj, akisema"Ninafikiri Makkah unabidi uwe mji wa waislam wote. Faida zinazopatikana kutokana na Hijja zinabidi zigawanywe kwa umma wote wa waislamu, na sio kwa nchi moja maalum tu. Fedha zinazopatikana kutoka Hijja zinabidi zigharimie miradi, mfano kuwasaidia watu nchini Somalia."Ameandika Hajji mmoja.

Haji mmoja wa kizungu ameelezea hisia zake kwa kiingereza kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, akionyesha picha na maelezo kutoka simu yake ya Smartphone. Al-Qaaba, Mina, Arafat na Muzdalifa ndio vituo ambavyo mahujaji wanabidi wapitie. Kila kimoja kiko mbali na chengine. Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook anaandika amefika katika kituo gani na kutoa ushauri kuhusu mahala pa kulala, saa ngapi wataondoka kwenda kituo chengine na njia gani ya usafiri ni bora zaidi. Kwa namna hiyo mahujaj wanaotumia simu za Smartphone watapunguza gharama.

Flash-Galerie Muslimische Pilger am Berg Arafat

Mlima Arafat-kilele cha Hajj

Hata Apple wamejitokeza na mtandao wao maalum kwa ajili ya mahujaji kwa jina iPhone-Islam. Mahujaj wanaweza kuutumia mtandao huo bila ya malipo. Mojawapo ya yaliyomo ni pamoja na Sala wakati wa Hajj.

Viongozi wa Saud Arabia pia wanautumia mtandao wa kijamii kuwasaidia mahujaji. Kwa namna hiyo maafisa wanawapatia mahujaji maaelezo wanayaohitaji na kadhalika.

Mwandishi:Ali Almakhlafi/Hamidou Oummilkhheir

Mhariri: Miraji Othman

 • Tarehe 04.11.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/134yP
 • Tarehe 04.11.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/134yP