1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magufuli aitaka TAKUKURU kuharakisha kesi za rushwa

Yusra Buwayhid
25 Agosti 2017

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameita taasisi ya kuzuwia na kupambana na rushwa nchini humo TAKUKURU kuharakisha uchunguzi na uendeshaji wa kesi za rushwa.

https://p.dw.com/p/2iqsk

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, wiki hii alimteua Brigedia Jenerali John Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU). Akizungumza baada ya kumuapisha jenerali huyo, Magufuli alikemea kudorora kwa kasi ya uchunguzi na uendeshaji wa mashtaka ya kesi zinazohusu rushwa na kuitaka taasisi ya TAKUKURU kuziendesha kesi hizo kwa haraka zaidi. Yusra Buwayhid anazungumza na meneja Mawasiliano wa taasisi hiyo, Mussa Misalaba, kutaka kujua ni kipi kipya kitafanywa na taasisi yao baada ya kauli ya Rais Pombe Magufuli. Bonyeza alama ya kisikilizo kusikiliza mahojiano hayo.