1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana dhidi ya chama cha AfD Ujerumani

Amina Mjahid
21 Januari 2024

Maelfu ya watu wameandamana tena dhidi ya chama cha siasa kali kisichopenda wageni AfD, baada ya kugundulika kuwa wanachama wa chama hicho walijadili kuhusu mipango ya kuwafukuza wageni Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4bVoa
Deutschland Frankfurt | Demonstration gegen AfD und Rechtsextremismus
Picha: Michael Probst/AP Photo/picture alliance

 

Waandamanaji walikusanyika nje ya bunge la Ujerumani mjini Berlin na pia katika miji kadhaa ya Mashariki mwa Ujerumani ambayo ndio ngome ya chama hicho cha Alternative für Deutschland au chama mbadala kwa Ujerumani. Waandamanaji wanaripotiwa kubeba mabango yalioandikwa "Wanazi nje"

Hapo jana zaidi ya waandamanaji 250,000 walikusanyika katika miji mbali mbali nchini Ujerumani yalikoitishwa maandamano hayo.

Hofu ya "fashisti" kuongoza serikali ya jimbo Ujerumani

Jioni hii maelfu wanatarajiwa katika maandamano ya  Munich, Berlin na Cologne kupinga sera za chama hicho, hii ikiwa ni kulingana na kituo cha televisheni cha Ujerumani ARD. 

AfD kilithibitisha juu ya wanachama wake kushirikicmkutano huo lakini kimekanusha kilijadili mpango wa kuwafukuza wageni Ujerumani unaodaiwa kupangwa na Martin Sellner, raia wa Austria ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la mrengo wa siasa za chuki dhidi ya wahamiaji barani Ulaya.