Mada tatu kuu zimechambuliwa na wahariri | Magazetini | DW | 31.10.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Mada tatu kuu zimechambuliwa na wahariri

Malipo jumla kwa masafa ya kwenda kazini na kurudi,kupungua idadi ya wasiokua na ajira ni miongoni mada magazetini hii leo

Tarakimu mpya katika soko la ajira ,uamuzi wa shirikisho la kabumbu la kimataifa FIFA,michauno ya fainali ya kombe la dunia,upande wa wanawake,ifanyike mwaka 2011 nchini Ujerumani,ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.Kwanza lakini tuumulike mjadala kuhusu marekebisho ya kile kijulikanacho kama “malipo jumla ya masafa kati ya mahala mtu anakoishi na kule anakofanya kazi.”

Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linaandika:

„Katika wakati ambapo msimamo rasmi wa waziri wa fedha unaonyesha umesalia kama zamani,kindani ndani anaonyesha kuridhia kuzingatia njia tofauti za kuanza upya kufanya kazi mfumo wa „malipo jumla ya masafa kati ya mahala mtu anakoishi na kule anakofanya kazi.Pengine kuregeza kamba huko ni mbinu tuu za uchaguzi.Zinaweza lakini kuathiri vibaya sana sifa ya waziri Peer Steinbrück.Kwanza,pengine hata asifanikiwe kupata njia mpya ambayo haitagharimu mafedha chungu nzima kwa serikali-na pili ataonekana kana kwamba hawezi kustahamilia vishindo vya nguvu“

Hayo ni maoni ya SÜDDEUTSCHE ZEITUNG,lakini hata FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEUITUNG lina maoni sawa na hayo .Gazeti linaandika:

„Mamilioni ya watu wanaokwenda na kurudi,masafa marefu kati ya kazini na nyumbani wanataraji watapunguziwa kodi ya mapato.Kama matarajio hayo yatatekelezwa-itategemea kadhia ya mtu mmoja mmoja.Mbali na kutathmini usumbufu wa kila mmoja,serikali ya muungano wa vyama vikuu italazimika kujibu masuala ya kimsingi ya sheria za malipo ya kodi za mapato-kama kifungu cha mageuzi kifutiliwe mbali , na badala yake kitumike kile kinachotaja masafa yanaanzia mlangoni mwa mahala mtu anakofanya kazi na sio ,mtu anapotoka nyumbani kwake kwenda kazini.Kuna hoja zinazounga mkono utaratibu asilia.Uamuzi uliowahi kupitiishwa na korti kuu ya sheria unasema:”Bila ya kazi hakuna gharama za usafiri.”Kwa namna hiyo,ni sawa,mwenyekwenda kazini mahala pa mbali hawezi kuepukana na gharama ambazo zinabidi zizingatiwe .”

Korti kuu ya mjini Karlsruhe inasubiriwa kupitisha uamuzi kama “malipo jumla ya masafa ya mahala mtu anakloishi na kule anakofanya kazi yaendelezwe au yarekebishwe.M ada nyengine magazetini hii leo ni kuhusu kupungua idadi ya wasio kua na kazi nchini Ujerumani.Gazeti la DIE WELT linaandika:

“Kiroja kikubwa hiki kuona jinsi SPD na vyama ndugu vya CDU/CSU wanavyodai hali nzuri katika soko la ajira ni matokeo ya siasa yao.Kiroja kwasababu hasa wao,SPD,na vyama ndugu vya CDU/SCU hawakufanya lolote la maana kuhimiza ukuaji bwa kiuchumi.Hali hii imesababishwa zaidi na hali ya kiuchumi namna ilivyo ulimwenguni.Kwamba soko la ajira la Ujerumani linafaidika na hali hiyo,cha kushukuriwa ni mageuzi yaliyotiwa njiani na serikali ya muungano wa vyama vya SPD na walinzi wa mazingira ya kansela wa zamani Gerhard Schröder.Sifa zinawaendeya wana SPD,walinzi wa mazingira na wana Union pia waliounga mkono kidogo mageuzi hayo.Kwa hivyo serikali ya muungano wa vyama vikuu mjini Berlin wasijisifu kwa kitu ambacho wao sio sababu.Wanabidi watahadhari ukuaji huu wa kiuchumi usije ukapooza watakapotaka kurejesha nyuma kile kinachoanza kuleta tija.”

 • Tarehe 31.10.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/C7l5
 • Tarehe 31.10.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/C7l5