1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUBUMBASHI:Makamanda wa nchi za maziwa makuu wakubaliana

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKl

Wakuu wa majeshi wa nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamekubaliana kushirikiana katika kuimarisha usalama kwenye maeneo ya mipaka ya nchi hizo.

Wakuu hao walisema kuwa wamekubaliana kuunda timu ya pamoja itakayokuwa na jukumu la kutathmini nyendo za makundi ya watu wenye silaha kwenye eneo hilo.

Wakuu wa majeshi wa nchi hizo wamekuwa wakikutana toka mwaka 2004 chini mwavuli wa Marekani kujaribu kuweka mikakati ya kijeshi dhidi ya makundi ya watu wenye silaha haswa katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo.

Wakati huo huo taarifa kutoka eneo hilo zinasema kuwa waasi wa kihutu wamekuwa wakishirikiana na majeshi ya serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo kupambana na kiongozi wa waasi wengine Generali Laurent Nkunda.

Nkunda amekuwa akidai kuwalinda watu wa kabila la Banyamulenge.