1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Chiluba apatikana na hatia ya wizi

5 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4b

Aliekuwa rais wa Zambia bwana Frederic Chiluba amepatikana na hatia ya wizi wa fedha kiasi cha dola milioni 46 na mahakama ya Uingereza.

Lakini msemaji wa bwana Chiluba ameliambia gazeti moja la Zambia kwamba raisi huyo wa zamani hatambui mamlaka ya mahakama hayo.

Bwana Chiluba alifanyiwa kesi hiyo nchini Uingereza kwa niaba ya mwanasheria mkuu wa Zambia.

Bwana Chiluba mwenyewe hakuwapo kwenye mahakama lakini uamuzi unaamanisha kuwa anaweza kunyang’anywa mali zake.