London.Aliyekuwa mpelelezi wa Kirusi yupo katika hali mbaya. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

London.Aliyekuwa mpelelezi wa Kirusi yupo katika hali mbaya.

Hali ya mpelelezi wa zamani wa Urusi aliyelazwa katika Hospitali mjini London kwa kile kinachodhaniwa kuwa amepewa sumu sasa inatajwa kuwa mbaya zaidi.

Rafiki wa Alexander Litvinenko amesema, mnamo majira ya usiku alikuwa akikabiliwa na matatizo ya moyo ambapo hivi sasa anasaidiwa kwa mashine za kumsaidia uhai.

Taarifa za vyombo vya habari zimesema, madaktari waliokuwa wakimshughulikia wamegundua vitu vya maajabu tumboni mwa mpelelezi huyo.

Litvinenko alisema kuwa alijisikia kuumwa baada ya kukutana na watu wawili wa Kirusi katika hoteli mnamo November Mosi.

Haijawekwa wazi hadi hivi sasa juu ya sumu aina gani aliyopewa lakini wataalamu wa masuala ya sumu wanadhani kuwa, sumu aina ya Thalium imetumika katika mkasa huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com