1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Wanajeshi wa Kingereza wauawa na bomu la Marekani

25 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBW8

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imearifu kuwa wanajeshi wake 3 wameuawa na 2 wamejeruhiwa katika wilaya ya Helmand kusini mwa Afghanistan. Waingereza hao waliuawa siku ya Alkhamisi baada ya kupigwa na bomu lililoangushwa na ndege ya kijeshi ya Marekani,ambayo iliitwa kuwasaidia wanajeshi wa Kingereza waliokuwa wakipambana na wanamgambo wa Kitaliban.

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Des Brown amesema tukio hilo linachunguzwa kwa makini.Itachukua muda kujua hasa kilichotokea,lakini ameahidi kuwa kutafanywa uchunguzi kamilifu.

Baada ya vifo hivyo vipya,Uingereza sasa kwa jumla imepoteza wanajeshi 73 nchini Irak tangu nchi hiyo kuvamiwa mwaka 2001 chini ya uongozi wa Marekani.