1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Vibali vya muda vya kazi kwa Wabulgaria na Warumania

22 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0J

Serikali ya Uingereza inataka kuweka vikomo kuhusu Wabulgaria na Warumania watakaotaka kusafiri Uingereza baada ya nchi zao kuwa wanachama katika Umoja wa Ulaya mwaka 2007.Vyombo vya habari nchini Uingereza vimesema,serikali ya London inatazamia kutoa vibali vya kazi vya muda tu.Vibali hivyo,vitatolewa kwa wafanyakazi walio na elimu maalum.