LONDON: uhusiano baina ya Uingereza na Marekani kuendelea kama ulivyo | Habari za Ulimwengu | DW | 15.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: uhusiano baina ya Uingereza na Marekani kuendelea kama ulivyo

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband amesisitiza kuwa uhusiano baina ya nchi yake na Marekani utaendelea kama ulivyo.

Waziri Miliband amesema hayo kufuatia kauli za mawaziri wengine wawili zilizoashiria kuwa uhusiano huo sasa umekuwa baridi.

Lakini bwana Miliband ameeleza kuwa hapatakuwa na mabadiliko katika mwelekeo wa waziri mkuu wa hapo awali bwana Tony Blair juu ya uhusiano huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com