1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON:Umoja wa Ulaya na Brazili zatia saini makubaliano ya kimkakati

5 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBle

Umoja wa Ulaya na Brazil zimetia saini makubaliano ya kimkakati katika mkutano wao wa kwanza wa kilele mjini Lisbon nchini Ureno.

Pande hizo mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta za siasa na uchumi, pia zinataka kushirikiana katika maswala ya kuhifadhi hali ya hewa na mageuzi ya taasisi za umoja wa mataifa.

Umoja wa Ulaya umetia saini makubaliano kama hayo na nchi chache tu ikiwa ni pamoja na Marekani, Canada, Urusi, China, India na Afrika Kusini.