1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ligi mashuhuri za ulaya ziko uwanjani.

29 Februari 2008

Hatima ya Hearts of Oak (Ghana) na union Douala kuamuliwa mwishoni mwa wiki hii katika kombe la klabu bingwa.

https://p.dw.com/p/DFnx

Kinyan’ganyiro cha kombe la klabu bingwa barani Afrika kimerudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii huku timu ya wanajeshi wa Gabon FC 105 ikila kiapo kutamba mbele ya mabingwa wa zamani Hearts of Oak ya Ghana. Sawa na Hearts of Oak ,mabingwa wengine Union Douala wamekuwa hatarini pia kupigwa kumbo. Nigeria imejipatia kocha mpya nae anatoka n yumbani james Peters akijaza pengo lililoachwa na Berti Vogts alieiongoza Nigeria mwezi uliopita katika Kombe la Afrika nchini Ghana na baadae kun’gatuka.

Liberia inajipatia kocha wa kijerumani.

Shirikisho la dimba la Ethiopia limeupinga uamuzi wa FIFA wa kumnrejesha madarakani rais wa shirika la dimba la Ethiopia waliomtimua.

Katika medani ya riadha, Kenya iliahidi kutokata rufaa dhidi ya adhabu ya marufuku ya mwaka mmoja aliopitishiwa bingwa mara 3 wa dunia wa mbio za nusu-marathon Susan Chepkemei.

Jumla ya mapambano 23 yanachezwa mwishoni mwa wiki hii katika Kombe la Afrika la klabu bingwa .Hearts of Oak ya Ghana waliotwaa kombe hili mara ya mwisho miaka 8 iliopita walikandikwa mabao 3-0 mjini Libreville, na wanajeshi wa FC 105 wa Gabon ambao wameapa kuwapiga kumbo kabisa kwao mjini Accra.Jumapili iliopita, Hearts of oak ilizabwa mabao 2:0 na Real Tamale United katika Ligi ya Ghana nah ii si ishara nzuri kabla ya changamoto za mwishoni mwa wiki hii.

Wenazo Union Douala huko Kamerun waliobidi kufuta mabao 3-1 waliochapwa na ASKO kara ya Togo ,lakini kikosi chao hikioneshi kinazihimili zahama za watogo Asko Kara.Kwani kiko mbali na ile timu yao iliotoroka na kombe 1979 hadi Douala.

Mabingwa mara 5 Zamalek ya Misri wako nyumbani baada ya kuondoka kigali duru ya kwanza kwa ushindi wa mabao 2:1 dhidi ya APR FC . Tunisia Club Africain pia haikuwa na wasi wasi kabla ya kukutana tena na Saloum – ya Senegal inayoshiriki kwa mara ya kwanza katika kombe hili .

Timu 10 zinazocheza nyumbani mwishoni mwa wiki hii na ni pamoja na mabingwa wa Afrika kusini –Mamelodi Sundowns ambao licha ya kuilaza Miembeni ya Zanzibar huko Amani wiki 2 nyuma ,imemtimua kocha wao Gordon Igesund kutokana na kutocheza uzuri katika Ligi ya nyumbani.

Ama katika Ligi mashuhuri za Ulaya ,macho yalikodolewa mpambano kati ya viongozi wa ligi Bayern Munich na mahasimu wao Schalke 04.Ingawa Schalke ilimudu ushindi wa bao 1:0 nyumbani dhidi ya FC porto ya ureno katika champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya hivi maju,i iliteleza mara 2 katika Bundesliga .

Bayern Munich ikitaka kupanua mwanya wake kileleni kati yake na werder Bremen.

Kuna wanaodai hatima ya kocha wa Schalke, Mirko Slomka inategemea firimbi ya mwisho ya mpambano wa jioni hii.Kwani, baada ya kulazwa na Wolfsburg mabao 2-1,Schalke ilikumtwa bao 1-0 na Bayer Leverkusen mwishoni mwa juma lililopita.Kwa mashabiki na uongozi wa Schalke,maji yamezidi unga.Lakini kutamba mbele ya Bayern munich wakati huu si kazi rahisi.

Hatima ya Armin Veh kocha wa mabingwa Stuttgart pia iinanin ginia hewani .Stuttgart miadi leo ilikua huko mashariki mwa Ujerumani na Energie Cottbus.

Manchester United ina yakini kwamba mwishoe, itaziba mwanya wake na Arsenal London na kuipiku ili kutetea taji lake la ubingwa msimu huu.

Uongozi wa Arsenal kabla changamoto za leo ulipunguzwa hadi point 3 huku zikisalia duru 11 za Ligi. Arsenal ilimudu suluhu tu ya mabao 2:2 na Birmingham mwishoni mwa wiki iliopita wakati Manchester united iliizaba Newcastle mabao 5-1.

Katika la Liga-Ligi ya Spain,Real Madrid ilikua leo izuwie kuteremka mlima na kuepuka kupitwa na mahasimu wao FC Barcelona katika Ligi ya Spian.Uongozi wa Real kileleni kati yake na Barcelona, ilikwishafifia hadi pointi 2 kabla ya changamoto za mwishoni mwa wiki hii.Madrid ina pointi 56 kwa 54 za Barcelona inayotamba sasa tena na samba wa nyika Samuel Eto’o wa Kamerun.

Katika Serie A, Ligi ya Itali Inter Milan ingali ikiongoza wazi usoni na i taji lake la 3 mfululizo yaonesha haliko mashakani.As Roma iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi ilitoka sare bao 1-1 na Inter Milan juzi jumatano.Roma ina miadi na Parma na Juventtus iliopo nafasi ya 3 inacheza Fiorentina.AC Milan imerefusha mkataba wa mwanasoka bora wa mwaka wa dunia Kaka wa Brazil hadi 2013.

Ligi ya Ufaransa,imekumbwa mwishoni mwa wiki iliopita na visa vya ukabila na viongozi mashuhuri wa kispoti nchini Ufaransa ,wameungana kuupiga vita na kuutimua nje ya dimba la Ufaransa-makamo-bingwa wa dunia. Miongoni mwao ni mfaransa rais wa UEFA-shirikisho la dimba la Ulaya - Michel Platini,waziri wa michezo Bernard Laporte na rais wa Ligi ya Ufaransa Frederic Thiriez.Mwishoni mwa wiki iliopita –vijana-manazi-mambo-leo walitia dosari Ligi hiyo kwa kutoa saluti za kinazi uwanjani huko Lyon.

Tukibakia katika dimba, shirikisho la mpira la Nigeria (NFA) lilimteua kati ya wiki hii James Peters kuwa kocha wake mpya akijaza pengo aliloacha Berti Vogts,aliekua kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na Scotland.Berti aliachana na Nigeria baada ya Super eagles kupigwa kumbo katika robo-finali ya kombe lililopita la afrika la mataifa na mahasimu wao wa jadi Black Stars-Ghana.

Peters,alikua kocha-msaidizi pale Nigeria ilipofika finali ya ya kombe la Afrika la mataifa 1984 nchini Ivory Coast na pia aliwahi kuiongoza timu ya vijan a ya Nigeria.

Peters ataiongoza Nigeria hadi pale jukumu la Samson Siasia kama kocha wa timu ya olimpik ya Nigeria ikimalizika huko Beijing.Nigeria imebakisha mpambano 1 tu kushinda ili ikate tiketi yake ya dimba la olimpik hapo August. Siasia aliongoza timu ya chipukizi ya Nigeria chini ya umri wa miaka 20 hadi finali ya kombe la dunia la vijana miaka 3 iliopita na sifa zake zitaongezeka ikiwa ataiongoza Nigeria kutwaa medali ya dhahabu ya Olimpik huko Beijing.Nigeria ina miadi na Bafana bafana-Afrika Kusini hapo Machi 26 kuamua nani anakwenda Olimpik na nani abakia Afrika.

Shirikisho la kabumbu la Ethiopia kati ya wiki hii liliupinga uamuzi wa FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni la kumrudisha madarakani rais wa shirikisho lake waliomtimua.Mkutano mkuu wa EFA-shirikisho la dimba la Ethiopia lilimuondoa madarakani rais wake Ashber Woldegirogise hapo januari kutokana na kile walichokiita “rekodi mbaya” ya dimba la Ethiopia chini ya uongozi wake.

FIFA bado kutoa kauli yake.

RIADHA:

Kenya-taifa kuu la riadha barani Afrika likianza sasa kujiwinda upya kwa michezo ijayo ya olimpik na mbio za nyika za kimataifa baadae mwezi huu huko Scotland,imeamua kutokata rufaa kupinga marufuku ya mwaka mmoja aliowekewa wiki hii bingwa mara 3 wa dunia wa mbio za nusu-marathon za wanawake Susan Chepkemei.

Katibu mkuu wa chama cha riadha cha Kenya-David Okeyo alisema msichana huyo mwenye umri wa miaka 32 aliekutikana ametumia madawa hapo septemba mwaka jana ,ana bahati kutopewa adhabu kali.Hii ni kwa kuwa aliungama kwamba alikula dawa kutibu homa ya mapafu ambayo imeingiza kitu kisichoruhusiwa. “Chepkemei hakuficha kitu na ndio maana tumempa marufuku ya mwaka mmoja ya kutoshiriki mashindanoni.”-alisema David Okeyo.

Chepkemei anakuwa mwanariadha 3 wa Kenya kufanya madhambi ya doping mnamo miaka 2 iliopita.

.