1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lagos. Wapiganaji wataka mapato yatokanayo na mafuta.

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJ0

Wapiganaji nchini Nigeria wanaofanya harakati zao katika eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Niger Delta wamewaachia huru wafanyakazi wawili wa Kitaliani ambao walitekwa nyara tangu mwezi Desemba.

Waasi hao wa kundi la Movement for the Emancipation of the Niger Delta wamesema wataongeza mashambulizi yao katika vituo vya machimbo ya mafuta na pia wataongeza kampeni yao ya mashambulizi ya mabomu.

Kundi hilo linataka uwezo mkubwa zaidi wa kujitawala katika jimbo hilo la Niger Delta na wanataka mapato makubwa yanayopatikana kutokana na mafuta kutoka kwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta.