1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuunganishwa majeshi ya Ujerumani mbili.

3 Novemba 2009

Hadi nchi 2 za Ujerumani zilipoungana , kila moja kati ya nchi hizo mbili za Ujerumani, ilikuwa na Jeshi lake: Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, kulikuwa Jeshi la Bundeswehr lilokuwa na askari 585.000.

https://p.dw.com/p/KB5e
Mwanajeshi wa Jeshi la Ujerumani (Bundeswehr)Picha: AP

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani (GDR) kulikuwa na Jeshi la Taifa (NVA) na askari 75.000.

Mwishoee, kutoka majeshi 2 likawa Jeshi moja la Bundeswehr.Haukupita muda, Jeshi hilo likajitwika jukumu jipya:Kutoka Jeshi la ulinzi, liligeuka Jeshi la kuingilia kati kuzuwia migogoro.Nchi moja,lakini majeshi 2, hiyo ndio hali iliokuwapo Ujerumani katika robo ya mwisho ya mwaka 1990.Katika Ujerumani magharibi,Jeshi la Bundeswehr likifanya gwaride lake na huko Ujerumani Mashariki, Jeshi la Taifa ,kwa ufupi (NVA) likiandamana.

"Lilikuwa ndilo jukumu la kulipatia haraka ufumbuzi:kuwaunganisha wananchi pamoja ambao kwa miongo kadhaa ,walishika silaha wakiwa washirika wa mashirika tofauti ya ulinzi."

Alikumbusha spika wa Bunge la Ujerumani, Norbert Lammert. Kwa Jeshi la Taifa la Ujerumani mashariki,ilikuwa hatima yake iliwadia kuvunjwa kabisa.Jeshi la Bundeswehr la Ujerumani magharibi,likageuka Jeshi la Ujerumani nzima na likawaingiza ndani yake askari 18.000 kutoka Ujerumani mashariki ambao kwanza walifanyiwa uchunguzi maalumu wa yale waliotenda jeshini.

Majamadari na maadimeri wote pamoja na maafisa wa kijeshi walioshiriki kisiasa, walibidi kuachishwa kazi.Zana za kijeshi za Jeshi la Taifa la Ujerumani Mashariki kwa kadiri kubwa, ziliteketezwa.Jeshi la (Bundeswehr) likashika dhamana za ulinzi Ujerumani nzima na hata pia Ujerumani mashariki.

"Nakula kiapo,kulitumikia kwa dhati ,Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani na kulinda barabara haki na uhuru wa umma wa Ujerumani."

Jeshi la pamoja la Ujerumani-Bundeswehr,lilikuwa chombo imara kabisa lililochangia mno kutekeleza umoja nchini.Lakini, lilikuwa kubwa mno likiwa na hadi wanajeshi 600.000.Idadi hiyo ilipindukia mno kiwango kilichokubaliwa katika mkataba wa kuziunganisha nchi mbili za Ujerumani.

Kwa hivyo, mnamo miaka 10 iliofuatia kuungana, kiasi wanajeshi 10.000 walipunguzwa na kambi nyingi zikafungwa.Isitoshe, Bundeswehr, Jeshi la Ujerumani, likahitaji jukumu jipya la kufanya:hii ni kwa kuwa,hakujakuwa tena na adui upande wa kambi ya mashariki.

Aliyekuwa wakati ule waziri wa nje wa Ujerumani,Bw.Klaus Kinkel, alisema kwamba kutokana na "zawadi ya karne" - kuungana tena ,Ujerumani imejipatia zawadi nono kutokana na kumalizika kwa vita baridi kati ya kambi ya magharibi na mashariki.Hata katika siasa za nje na ulinzi, aliongeza, waziri huyo,kulihitajika fikra na mawazo mapya.Kipindi cha endapo ikiwa hivi ,itakuwa vile kimepita-alisema Bw.Kinkel.

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Mhariri: Abdul-Rahman